1 / 2

MATUKIO MUHIMU KATIKA TEKNOLOJIA – MAONI KUTOKA KUTOKA KWA WAKEMIA

II. HABARI NA MAWASILIANO. MATUKIO MUHIMU KATIKA TEKNOLOJIA – MAONI KUTOKA KUTOKA KWA WAKEMIA. Uvumbuzi katika kemia, uhandisi na elektroniki mwishoni mwa karne ya 19 na kuendelea hadi sasa umetuwezesha kurahisisha mawasiliano kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

lesa
Download Presentation

MATUKIO MUHIMU KATIKA TEKNOLOJIA – MAONI KUTOKA KUTOKA KWA WAKEMIA

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. II.HABARI NA MAWASILIANO MATUKIO MUHIMU KATIKA TEKNOLOJIA – MAONI KUTOKA KUTOKA KWA WAKEMIA Uvumbuzi katika kemia, uhandisi na elektroniki mwishoni mwa karne ya 19 na kuendelea hadi sasa umetuwezesha kurahisisha mawasiliano kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Maisha yetu yamebadilika sana kutoka karne iliyopita, kutoka maisha ya vijijini hadi mijini, kutoka kwa jamii ya wasomi hadi elimu kwa umma, kutoka kilimo hadi kazi za utafiti. Maingiliano ya watu, habari, mawazo mapya na mabadiliko ya vifaa mbali mbali imepelekea mabadiliko makubwa ya kijamii duniani. Matukio mbali mbali ya kemia yamechangia katika maendeleo katika nyanja mbali mbali za mawasiliano ikiwemo zile tunazohitaji kuona, kuhifadhi pamoja na kusambza kwa wengine. Mawasiliano kwa njia zisizotumia waya (wireless communcation) na yale yakutumia mkongo (fiber optic) ni kielelezo cha kuanza kuvumbuliwa na kutumika kwa intaneti (internet). Matumizi ya metali za silikoni (silicon) katika kemia pamoja na muungano wa nguvu za polima (polymers) imepelekea kuvumbuliwa kwa kompyuta hizi tunazotumia sasa. Michezo ya sinema (movies), televisheni (television) na picha – vyote hivi hutegemea kemia ambayo husaidia pia kuhifadhi kumbukumbu katika nyanja hii. Mafanikio ya kisayansi katika kemia yamepelekea jamii zinazoishi mbali mbali vijijini kuweza kuwasiliana na wengine sehemu zozote duniani. II. 1. Mawasiliano(Communications Advances) Maendeleo katika sekta za simu Mawasilianoyasiyotegmea waya Faksi na zerografi Mkongo wa mawasiliano II.2. Teknolojia ya Kompyuta (Computer Technology) Kuvumbuliwa kwa kompyuta Teknolojia ya vitoa-moto Kibanzi cha silikoni na saketi ndogo inayounganisha vitu vingi Skirini na teknolojia ya maonyesho Ghala ya kuhifadhia habari Satalaiti za mawasiliano II.3. Burudani (Entertainment Developments) Senema Televisheni Picha II. 4. Uvumbuzi katika Elektroniki (Innovations in Electronics) Uvumbuzi katika matumizi ya elektroniki Teknolojia ya kutengeneza vifaa mbadala (vya plastiki ngumu) Transista

  2. II. HABARI NA MAWASILIANO Matukio: 1876 Alexander Graham Bell akamilisha mtambo wa kwanza wa simu. 1926 The Warner brothers yakamilisha kutengeneza senema ya kwanza iliyotumia kwa pamoja muziki pamoja maongezi. 1926 Njia mbili za maongezi kuvuka bahari ya Atlantiki zaanza kutumika kwa mara ya kwanza. 1927 Philo T. Farnsworth aanza matangazo ya televisheni kwa kutumia mionzi ya cathode (cathode ray tube). 1946 ENIAC, kompyuta ya kwanza katika mfumo wa dijitali (digital) yaanza kutumika. Mhangari, John von Neumann ni miongoni mwa wanasayansi waliofanyia mabadiliko mfumo hesabati katika ENIAC. 1947 Transista yavumbuliwa katika maabara ya simu ya Bell Telephone. 1955 Reynold Johnson aboresha disketi (disk drive) ya kwanza duniani. 1958 Jack Kilby wa Texas Instruments avumbua saketi ndogo inayounganisha vitu vingi (integrated circuit (IC)). 1961 Kibanzi cha metali ya silikoni (silicon chips) chaanza kutumika. 1961 Telstar, satalaiti ya kwanza yatumwa katika njia ya mzunguko wa dunia (obiti – orbit). 1961 Kampuni ya Eastman Kodak yazindua kamera ya Instamatic ambayo ina filamu. 1971Kampuni ya Intel yazindua kompyuta yenye kutumia mfumo wa 4004 4-bit maikroprosesa (microprocessor) kwa wateja. 1977Chicago yazindua kwa mara ya kwanza mfumo mkongo wa mawasiliano (fiber-optic communications system). 1983 Simu za mikononi (cellular phones) zapata umaarufu kutokana na mawasiliano yake kutounganishwa na waya. 1984 CD-ROM (compact-disc-read-only memory) yavumbuliwa sambamba na compact disc (CD) za kawaida. A. Graham Bell Senema ya kwanza,The Jazz Singer, inayotumia muziki pamoja na maongezi. Philo T. Farnsworth na mirija ya mionzi ya cathode (cathode raytube) ENIAC Transista ya kwanza duniani. Kibanzi cha silikoni (silicon chip) Saketi ya kwanza ndogo inayounganisha vitu vingi. Kodak-Instamatic Telstar Mkongo wa mawasiliano (fiber optics) ukisambazwa kwa mara ya kwanza Chicago The Intel’s 4004 4-bit prosesa (processor)

More Related