80 likes | 476 Views
III.1. Udhibiti wa Maumivu Makali na Uvimbe. Morphine (Morphine)
E N D
III.1. Udhibiti wa Maumivu Makali na Uvimbe Morphine (Morphine) Imeanza kutumika katika miaka ya 1800 kupunguza hisia za maumivu makali, morphine hutokana na mimea ya kasumba (afyuni) (opium). Mfamasia kutoka Hungary Janos Kabay alizindua uzalishaji wa morphine katika miaka ya 1920 kutokana na utomvu wa mimea isiyokomaa ya kasumba (poppy-head). Mfumo kemikali wa morphine ulifanyiwa utafiti mwaka 1923 kwa lengo la kuondosha magonjwa ya wasiwasi, maumivu makali pamoja na uchovu. Kwa kufahamu athari za magonjwa hayo kwa binaadamu pamoja na umuhimu wa dawa hizo, dawa hizo ziliboreshwa na kutengenezwa dawa ziitwazo nalorphine na naloxone mnamo mwaka 1961. III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA Sanamu la Janos Kabay, Budapest, Hungary Aspirini (Aspirin) Mnamo mwaka 1890, tindikali za salicyclic(salicyclic acid) zilianza kutengenezwa na kuwa tiba ya magonjwa makali ya maumivu, maumivu makali ya viungo pamoja na matatizo ya uvimbe, ziliendelea kutumika licha ya athari zake kadhaa zilizogundulika baadae kutokana na dawa hizo (nausea, gastric catarrh). Acetylsalicyclic acid (Aspirin) iligunduliwa mwaka 1897 na Mkemia wa Kijerumani, Heinrich Dreser. Uzalishaji rasmi mwaka 1899 na dawa ya kwanza kuuzwa mwaka 1900. Aspirin ilipata umaarufu kutokana na kutokuwa na athari nyingi kulinganisha na salicylic acid. Aspirin ilikuwa ni dawa ya kwaza kuanza kuzalishwa kwa wingi viwandani, hadi sasa yaendelea kuzalishwa kwa kiwango kikubwa. Aspirin, dawa iliyotumika kwa maumivu makali ya kichwa hadi katika miaka ya kati ya 1980, wakati faida zake zilipoongezeka zaidi na kuwa kinga ya magonjwa ya moyo. Acetylsalicylic acid Cortisone (Cortisone) Mnamo miaka ya 1940, tafiti kuhusu tezi za adrenali(adrenal gland cortex) zimethibitisha kuwepo kwa baadhi ya homoni (hormones) ambazo pia hujulikana kwa jina la steroids (steroids) kutokana na uwezo wake wa kuhimili maumivu makali. Tafiti za kwanza zilianza mwaka 1936 kwa kuweza kuiengua kutoka katika sehemu yake asilia, dawa zenye adrenali (cortisone) baadae zilithibitishwa na Mkemia wa Kimarekani Lewis Hastings Sarett mwaka 1948 na kuingia katika soko mwaka mmoja baadae baada ya maajabu yalioonekana katika dawa hizo kwa kutibu kwa uhakika magonjwa ya yabisi kavu (arthritis) na baridi yabisi (rheumatoid arthritis). Hata hivyo, tafiti za tiba baadae ziligundua kwamba ingawa cortisone haitibu moja kwa moja yabisi kavu (arthritis) pamoja na kujitokeza athari kadhaa za matumizi ya dawa hizo lakini imekuwa dawa maridhawa kwa magonjwa ya pumu pamoja na magonjwa ya athari nyengine za vijisumu (allergy). Tafiti nyengine kuhusiana na steroids zimepelekea kugunduliwa kwa madawa zaidi kama prednisone, prednisolone na dexamethasone ambayo ni mwafaka katika tiba ya magonjwa ya maumivu makali ya viungo na yasiyokuwa naathari kubwa mwilini. Lewis Hastings Sarett Kupanguka kwa viungo kunakosababishwa na maumivu makali na yabisi.
III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA III.2. Tiba ya Magonjwa ya Akili Chlorpromazine (Chlorpromazine) Chlorpromazine (Thorazine, Hibernal) kwa mara ya kwanza ilitumika kutibu magonjwa ya akili, schizophrenia mwaka 1954, baada ya kutengenezwa katika tiba ya magonjwa ya athari za histamine. Tiba hii imethibitika kuwa ni ya mafanikio zaidi hasa katika kipindi cha uvumbuzi wa tiba za magonjwa ya akili. Udhibiti wa magonjwa ya akili kwa kutumia madawa ya uhakika umechukua nafasi ya mfumo wa tiba za magonjwa hayo uliozoeleka awali kama vile; electroshock, insulin shock na prefrontal lobotomy (upasuaji) na kusaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa kasi asilia ya ongezeko la magonjwa hayo. Baadae tafiti zaidi zimeonyesha kwamba tiba ya kutumia chlorpromazine imefanikiwa katika magonjwa ya akili kwa kuweza kuvumbuliwa dawa nyengine bora zaidi za Halopridol na Olanzapine. Picha kutoka katika filamu:One Flew Over the Cuckoo’s Nest(1975), ambayo huonyesha athari za magonjwa ya akili Tiba ya kuondosha ugonjwa wa wasiwasi (Tricyclic antidepressants) Mnamo mwaka 1958, utafiti katika nyanja ya tiba uligundua dawa iitwayo Imipramine, dawa ambayo asili yake ilikuwa ni tiba ya magonjwa ya akili, imethibitishwa pia kuwa yaweza kuwa tiba pia ya kuondosha ugonjwa wa wasiwasi. Kazi yake kubwa ni kutibu mwenendo wa hisia (neurotransmitters) katika ubongo. Dawa kadhaa zilizogunduliwa na kuboreshwa baadae katika mfumo huu hujulikana kwa pamoja kama ni, ’tricyclic’ – tiba ya kuondosha magonjwa ya wasiwasi. Tricyclic antidepressants imethibitishwa baadae kuwa ni tiba ya magonjwa haya thakili. Athari za shinikizo la moyo (depression) wakati wa kujifungua Benzodiazepines (Benzodiazepines) Mnamo mwaka 1959, Chlordiazepoxide (Librium) ilizindua dawa mpya, benzodiazepines yenye kutuliza magonjwa ya akili na wasiwasi. Dawa hii ilichukuwa nafasi ya dawa zilizozoeleka za usingizi na Meprobamate zilizogunduliwa mwaka 1950 ambazo awali zilionyesha mafanikio kama kitulizo cha wasiwasi na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi katika kipindi hicho cha kuvumbuliwa kwake. Benzodiazepines methibitika kwa ubora na salama kwa matumizi yake ikia ni pamoja na tiba ya kutuliza kukacha kwa misuli pamoja na magonjwa ya kifafa. Mwenendo wa hisia (neurotransmitters) katika ubongo.
III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA III.3. Homoni na Kirekebishi Homoni Insulini (Insulin) Insulini, homoni za protini zinazotengenezwa kwa chembechembe maalum za wengu (pancreas) ili kudhibiti kiwango cha sukari katika damu mwilini. Uhaba wa insulini huchangia kupatikana kwa ugonjwa wa kisukari (diabetes), ugonjwa uliosababisha maafa makubwa kwa binaadamu hadi katika miaka ya 1920. Madaktari wawili wa Canada, Frederick Banting na Charles H. Best waligundua tiba ya sindano kutokana na chembechembe za wengu (bovine pancreas) mwaka 1921. Mgonjwa wao wa kwanza alikuwa ni mtoto wa miaka 14 ambaye alikuwa mahututi alishatolewa hospitali baada ya madaktari kushindwa kumpatia tiba ya kufaa. Insulini imeanza kutengenezwa kutokana na chembechembe za wengu na kampuni ya Eli Lilly mnamo mwaka 1922. Insulini ya kwanza kutengenezwa kutokana na mchanganyiko wa teknolojia ya DNA ilianza kutumika mwaka 1982. Michoro ya Frederick Banting na Charles H. Best Testosterone (Testosterone) Testosterone ni dawa za kuongeza nguvu za uzazi kwa mwanamme na ni imara katika kuongeza nguvu za tendo la ndoa kwa mwamume. Ni jamii za homoni za steroid ambazo zinafanana na jamii ya kolestroli. Testosterone ziligunduliwa kwa mara ya kwanza katika kolestroli mwaka 1935 kutibu ugonjwa wa unyaufu wa homoni. Testosterone yaweza kutengenezwa kwa kemikali au chembechembe za maikrobiolojia (microbiological modifications) ambazo pia zaweza kupatikana katika vitu vya mazingira halisi. Projestini, estrojini na dawa za uzazi wa mpangilio(Progestins, estrogens and oral contraceptives) Katika miaka ya 1930, homoni (hormones) mbili za kike zilitolewa na kukuzwa kutoka katika mazingira yake asilia, mkojo wa farasi jike mwenye mimba na viazi (Mexican sweet root). Projestini (progestrone, luteal hormone) ziligunduliwa kuwezesha mimba na estrojeni (follicular hormones) imethibitika kuwa huathiri mzunguko wa hedhi kwa mwanamke. Katika miaka ya 1950 tafiti zaidi za homoni zilifanywa zikiwemo zinazohusu utungaji wa mimba na athari zake. Hatua kubwa iliyofikiwa ikiwemo uvumbuzi wa dawa za uzazi wa mpangilio kwa wanawake. Dawa za Envoid zilizokuwa na soko kubwa nchini Marekani katika miaka ya 1960 zilikuwa ni dawa za mwanzo za uzazi wa mpangilio kuvumbuliwa zikiwa na mchanganyiko wa estrojini (estrogens) na progestini (progestins) ambazo hazikuwa na madhara kwa binaadamu. III.4. Tiba za Vidonda vya Tumbo Ugunduzi wa tiba ya vidonda vya tumbo (Evolution of ulcer therapy) Mnamo mwaka 1972, James Black, mtaalamu wa kiskochi (Scotland) na wenzake akina Smith, Kline na French walibainisha kuwemo kwa tindikali hatari ndani ya tumbo. Mwaka 1976 waligundua dawa iitwayo Cimetide (Tagamet) ambayo huikinga tindikali ili iwe na madhara duni ambapo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza haja ya upasuaji kwaajili ya tiba ya vidonda vya tumbo. Tagamet imejipatia umaarufu zaidi kwa tiba ya vidonda vya tumbo.
III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA III.5. Uchunguzi wa Afya na Magonjwa Teknolojia ya Taswira katika Tiba (Medical imaging technologies) Vifaa vya tiba kama mashine za picha za x-ray na MRI zimeboreshwa kulinganisha na wakati zilipovumbuliwa, sasa zimekuwa ni za kawaida katika ugunduzi na uchunguzi wa maradhi. Mwanafizikia wa Kijerumani Wilhelm Roentgen aligundua x-ray kwa mara ya kwanza mwaka 1895 alipopiga picha kugundua mifupa ya mkono wa mkewe. Teknolojia ya kinyuklia na sumaku (Nuclear Magnetic Resonance – NMR) ili kuweza kutambua mfumo kemikali iligunduliwa katika miaka ya 1970 na kipimo cha picha cha Magnetic Resonance Imaging kilithibitishwa kwa matumizi ya binaadamu mamo mwaka1985. Vipimo vyengine kemikali vikiwemo vile vya filamu kugundua magonjwa vimekuwa na mafanikio makubwa kama vile vipimo vya picha vya x-rays, CT (kipimo kinachofanya kazi za kupiga picha za x-ray wakati mmoja na msaada wa kompyuta), MRI pamoja na vipimo vya mashine ya kupiga picha sehemu za ndani ya mwili wa binaadam (ultra sound images). Kivuli cha mikono ya Ms.Roentgen Isotopu za Tiba (Medical isotopes) Matumizi ya michoro na vielelezo katika tiba zimepelekea kwa kiasi kikubwa kuweza kugunduliwa kwa isotopu (isotopes) za madawa na tiba ili kuweza kugundua utendaji kazi wa viungo vya ndani ya mwili wa viumbe kufuatia kazi kubwa ya ugunduzi iliyofanywa na mshindi wa nishani ya Nobel (1943), mwanasayansi wa Hungary, Georg Hevesy. Mwaka 1935 aliweza kugundua metabolism iitwayo phosphor metabolism kwa kutumia radioactive nuclides. Mchanganyiko unaofanywa kwa isotopu za radioactive (radioactive isotopes) kama vile technetium-99m na thalium-201 au matumizi ya radio-opaque (kama barium na iodine compounds). Baadae isotopu za radio-labeled compound huingizwa ndani ya mwili pamoja na kamera maalum (gamma-detecting cameras) ili kutoa picha na michoro ya ndani ya mwili. Dalili za awali za magonjwa mbali mbali zaweza kugundulika mapema kama magonjwa ya ini (liver disease) pamoja na vipimo vya dalili za awali za moyo kushindwa kufanya kazi (stress test for cardiac function). Maendeleo katika mchanganuo wa Kemikali (Development of chemical assays) Kwa sasa tumekuwa tukiweza kuelewa hali za afya na kujifunza kutokana na maradhi au mabaki ya madawa ambapo chembechembe zake zaweza kupatikana katika damu, mkojo, kinyesi, mate au hata pumzi. Vipimo katika maabara chini ya msaada wa kompyuta na hata katika vipimo vya kujiangalia afya nyumbani vimeweza kugundua mjengeko wa kemikali mbali mbali. Katika karne ya 19, kwa mfano, magonjwa yaliweza kufahamika kwa dalili za kiafya tu, kama mgonjwa atathibitika kuwa na ugonjwa unaohitaji tiba mwafaka pekee, hapo ndipo mtu huyo hubainika ama kuthibitishwa kuwa na ugonjwa husika. Uchunguzi wa maradhi ulianza mwaka 1882 wakati Paul Ehrlich alipogundua kuwa kuwepo kwa bekteria wanaosababisha homa ya matumbo waitwao typhoid bacillus ni ithibati ya ugonjwa wa homa ya matumbo (typhoid fever). Kabla maradhi hayo yaliweza kukisiwa tu kwa kuweza kuangaliwa rangi ya ngozi ya mgonjwa husika wa homa ya matumbo. Ugunduzi wa vifaa vya kujiangalia afya (Evolution of personal monitoring) Vifaa vya kujiangalia afya nyumbani vimeongeza umuhimu kwa binaadamu kujiangalia afya zao. Kwa mfano, wagonjwa wa kisukari ni mara chache sana kwenda katka maabara za hospitali kupima kiwango chao cha sukari kuwemo katika mkojo. Mnamo mwaka 1941, Miles Laboratories ilitengeneza kipimo cha kigundua sukari katika mkojo kwaajili ya matumizi ya nyumbani. Ingawa ilikuwa taabu kidogo kuweza kukiboresha kifaa hicho, hatimaye wataalamu hao walifanikiwa kugundua kifaa imara cha kuweza kusoma sukari katika mkojo mnamo mwaka 1956. Katika miaka ya 1960, kipimo cha mwanzo chenye kutumia betri kupima wagonjwa wa sukari kiligunduliwa, kikiwa mfano wa kijiti ambacho kimeweza kuokoa maisha na kuboresha afy kwa wagonjwa wa kisukari. Katika miaka ya 1970 na 1980 vifaa mbali mbali viligunduliwa ikiwemo kipima mimba, uovushaji (ovulation), mzunguko na kiwango cha damu na nyenginezo.
III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA III.6. Dawa za kutibu Maambukizi (Anti-infective Drugs) Salvarsan na Prontosil (Salvarsan and Prontosil) Paul Ehrlich, mtaalamu wa kijerumani katika masuala ya bekteria, wakati akitafiti michnganyiko tofauti ya sumu kwa lengo la kuua bekteria alivumbua dawa ya salvarsan mwaka 1909 ikiwa ni dawa ya kutibu magonjwa hatari ya zinaa, ikiwemo kaswende. Tafiti nyengine ziliendelea kufanywa na watafiti mbali mbali katika kupambana na maambukizi ya magonjwa kadhaa ikiwemo dawa ya mwanzo kuvumbuliwa yenye mchanganyo wa salfa (sulphur),Prontosil, ambayo awali ikitumika katika kutengeneza nguo iligunduliwa mwaka 1932 ambapo wakemia wakiendeleza tafiti mbali mbali za kutafuta dawa ya kupambana na maambukizi ya bekteria hatari waitwao streptococcal ambayo husababisha ugonjwa sugu wa homa za mapafu (chronic pneumonia). Utafiti huu ulikuwa ni muhimu sana hadi mvumbuzi wake Mkemia wa Kijerumani Gerhar Domagk kutunukiwa nishani ya Nobel kufuatia mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa dawa hizo za tiba. Dawa nyengine ya kuua bekteria sugu, Prontosil ilivumbuliwa baadae ikiwa ni mchanganyo wa sulphanilamide. Dawa nyengine kadhaa za kuua vijisumu mwilini ziligunduliwa baadae ikiwemo Sulphapyridine iliyogunduliwa mwaka 1938. Dawa za mchanganyo wa salfa zimeonyesha kuwa na mafanikio zaidi kwa kupunguza vifo vinavyosababishwa na homa ya mapafu katika miaka ya 1940 na kuokoa maisha ya mamilioni ya watu. Dawa hii ilianza kupoteza umaarufu baada ya kuvumbuliwa dawa ya Penicillin. Streptococcus bacteria Gerhard Domagk Prontosil Alexander Fleming Penicillin (Penicillin) Mnamo mwaka 1928, mtaalamu wa masuala ya bekteria wa Kiskochi (Scottish), Alexander Flemming aligundua dawa za kuua bekteria (Penicillium notatum). Penicillin, ni dawa zilizogunduliwa katika kipindi cha vita mwaka 1943, maalum kwa kutibu maambukizi pamoja na majeraha makubwa kwa askari wa Uingereza na Marekani wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. Dawa hii iliyokuwa ghali na adimu kupatikana ililazimika kutengenezwa upya kutoka katika mkojo wa wagonjwa wanaotumia dawa hizo. Wanakemia waligundua njia mpya ya kuitengeneza dawa hiyo: wakitumia njia za kienyeji na asilia zinazounda dawa hiyo. Muundo kemikali wa Penicillin ulivumbuliwa na mtafiti wa kiingereza, Dorothy Crowfoot Hodgkin katika miaka ya 1940. Kuanzia mwaka 1957, makampuni mbali mbali yalianza kutengeneza dawa hizo kwa biashara na kuwa miongoni mwa dawa zilizofanikiwa sana katika kuua vijisumu mwilini. Penicillium notatum Zidovudine (AZT) Zidovudine (AZT) imethibitishwa nchini Marekani kutibu maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini (HIV) mwaka 1987. Dawa hii iligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1964 lakini ikaonekana dhaifu kwa tibakemikali ya saratani. Ilizuiliwa hadi mwaka 1986 wakati tafiti mbali mbali za tiba zikiendelea nchini Marekani. AZT ina sifa ya kulenga hadi katika virusi maalum vilivyokusudiwa ndani ya mwili wa binaadamu. Kutokana na maendeleo ya tiba za maambukizi ya HIV, awali ilionekana kama AZT isingeliweza kupambana na maambukizi hayo ya HIV. Zidovudine crystals Zidovudine
III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA III.7. Uangalizi wa Mishipa ya Moyo (Cardiovascular Management) Udhibiti wa mapigo ya moyo Matumizi ya dawa aina ya Procaine kudhibiti mapigo ya moyo iligunduliwa katika miaka ya 1930. Dawa hii yenye matumizi ya utata kidogo kwasababu dawa hiyo ambayo huzuia mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida huweza kusababisha pia mapigo ya myo yasiyo ya kawaida katika mwili wa binaadamu. Procaine huzuia ugamba mwembamba wa chembe chembe hai za protini ambazo hujulikana kama sodium channels. Dawa nyengine kadhaa zimevumbuliwa baada ya Procaine zikiwemo beta-blockers na zile za jamii ya potashamu (potassium) na kalshamu (calcium). Tiba ya moyo kushindwa kufanya kazi Digitalis glycosides, dawa inayotokana na mchanganyiko wa mimea mbali mbali imanza kutumika kuwa tiba ya kuzuia moyo kushindwa kufanya kazi kwa karne nyingi sana. Baada ya tafiti mbali mbali kuthibitisha kwamba yaweza kuongeza kasi ya tiba ya magonjwa hayo, Digoxin kutoka katika majani ya mimea ya grecian foxglove (Digitalis lanata) na kuthibitishwa mwaka 1954 kwa tibaya magonjwa ya moyo. Imethibitishwa zaidi kwamba dawa ya kudhibiti mapigo ya moyo (anti-hypertensive) pia hutumika kama tiba ya moyo kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Tiba ya kuganda kwa damu Heparin, dawa inayotokana na ini la wanyama, ilianza kutumika kwa mara ya kwanza kama tiba ya kuganda kwa damu (thrombosis – blood cloting) wakati wa kutiwa damu (blood transfusion) mnamo mwaka 1935 na baadae ilianza kutumika rasmi katika tiba ya kuganda kwa damu, ambayo pia ilijulikana kama kilainishi cha damu (blood thinner). Huzuia mgando wa damu katika tiba ya upasuaji wa mishipa ya cardiac na arterial. Wafarin (Coumadin) dawa ya kukinga ugonjwa wa kupooza na kutibu ugonjwa wa moyo na kuganda kwa damu ilithibitishwa mwaka 1955. Urokinase, dawa inayotumia enzaimu (enzyme) kuyayusha kuganda kwa damu ilivumbuliwa mwaka 1977, Streptokinase iligunduliwa mwaka 1978 na Plasminogen activator (tPA) ilithibitishwa mwaka 1987. Udhibiti wa kiwango cha Kolestroli (cholestrol) katika damu Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kolestroli ndani ya mishipa ya damu (arteriosclerosis) ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayopelekea magonjwa ya moyo na kupooza (stroke). Lovastatin (Mevacor) ambacho hudhibiti kiwango cha kolestroli katika damu (hypolipemic activity) kwa kuingiza kiwango cha enzaimu na kubadilishwa kuwa mevalonate, kipimo cha kiwango anuwai cha kolestroli (cholestrol) kilitambuliwa mwaka 1987. Hata hivyo, dawa mbali mbali baadae ziligunduliwa kama Simvastatin na Atorvastatin zimeboreshwa ili kudhibiti kiwango kikubwa cha mafuta katika damu (hyperlipidemia) na kuonyesha mafanikio makubwa. Arterioschlerosis
III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA III.8. Tiba-kemikali ya Saratani (Cancer Chemotherapy) Uvumbuzi wa Tiba-kemikali ya Saratani Matumizi ya kemikali kwa kutibu saratani (cancer chemotherapy) ilianza mwaka 1942 kwa kutumia nitrojeni nyepesi na Louis S. Goodman na Alfred Gilman. Dawa ambazo huzuia tindikali za foliki (folic acid) ambazo pia hujulikana kama antimetabolites pia ziliboreshwa. Dawa za Aminopterin zilizogunduliwa mwaka 1947 zilikuwa bora zaidi katika kupambana na saratani ya damu (leukemia) lakini ziligundulika kuathiri kwa kasi chembechembe nyeupe za uhai katika damu (white blood cells) ilisitishwa na dawa ya Methotrexate kuchukua nafasi yake. Katika miaka ya 1950 George Hitchings na Charles Heidelberger waliiboresha dawa ya antimetabolitic mercaptopurine kwaajili ya saratani ya damu na Fluorouracil kwaajili ya magonjwa ya maumivu makali ya tumbo (gastrointestinal) na uvimbe katika matiti. Dawa ya Cytotoxic Cytotoxic (dawa ambayo ni sumu kwa chembechembe za mwilini) inatokana na miti ambayo kwa mara ya kwanza ilianza kutumika kama tibakemikali ya saratani mwaka 1963. Dawa hii ya kupambana na saratani hufanya kazi ya kuzuia ueneaji wa chembechembe za uhai kama vile neoplastiki (neoplastic) au saratani (cancerous). Dawa mbali mbali zikiwemo vinca alkaloids (vincristine na vinblastine) ambazo hutokana na mimea ya periwinkle na podaphylotoxin ambayo hutokana na mimea ya mayapple zilizovumbuliwa mwaka 1970. Taxol imevumbuliwa kutokana na mimea ya Pacific yew mnamo mwaka 1971 na kuboreshwa na kuwa tiba ya saratani na mapafu mwanzoni mwa miaka ya 1990. Tamoxifen (Tamoxifen) Tamaxifen, iligunduliwa mwaka 1971 na kuanza kutumika mwaka 1977 kama tiba ya saratani ya matiti (breast cancer) kwa kupunguza kasi ya ukuaji wa uvimbe wa estojeni (estrogen-dependent tumor). Ukuaji wa kiasi kikubwa wa estrojeni husaidia ukuaji wa chembechembe za uhai (cell) ambazo huenea hadi katika tishu (tissue) za matiti. Aina hii ya tibakemikali huzuia homoni (hormones) asilia ambazo huchangia aidi ukuaji wa chembechembe hai za saratani. Megestrol ni mnyambuliko wa homoni za steroidi (steroid hormone) na pregestroni (pregestrone) ambazo hutumika katika tiba ya uvimbe wa matiti. Michoro ya Mammographic kuonyesha uvimbe katika matiti Kujiangalia afya ya matiti kwa kuweza kugundua dalili za awali za saratani
III. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – AFYA NA MADAWA III.9. Vifaa vya Matunzo ya Afya Viungo bandia na Vifaa vya Afya Miguu ya bandia na viungo vingine bandia, vimechukua nafasi ya viungo asili, lenzi (lenses) za kuonea na vifaa vingine vya kusikia na vyengine vya tiba ya afya hutengenezwa kwa kutumia plastiki maalum na kwa utaalamu wa hali ya juu chini ya msaada mkubwa wa kemia. Kwa kuigizia vifaa vya asili na kuvitengeneza vyengine upya, kemia na wahandisi wameboresha vifaa vya tiba na kuwa imara na vya uhakika zaidi. Miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na uvumbuzi wa figo bandia (1945), mishipa bandia ya moyo iliyogunduliwa katika miaka ya 1950 pamoja na upandikizi wa moyo bandia, mwaka 1982. Lenzi za plastiki ziligunduliwa mwaka 1956 na baadae kufanyiwa marekebisho na kuwa nyepesi zaidi mnamo mwaka 1985. Valvu bandia za moyo Moyo bandia Vifaa vya Tiba Kemia imetumika katika matengenezo yote ya vifaa vya plastiki na vyengine vya madawa vinavyotumika katika hospitali na vituo vya afya. Vifaa vya kisasa vya afya ni lazima viwe imara kwa matumizi ya kila siku ambapo vitasaidia kuimarisha na kuhakikisha usafi wa vifaa hivyo, usalama pamoja na kutokuwa katika mazingira ya kutoweza kupata vijidudu vya maradhi. Nyanja ya afya huhitaji vifaa vya uhakika vikiwemo vya kugundua maradhi (diagnostic equipments), vipimo (stethoscopes), bendeji (bandages) na vifaa vingine zikiwemi sindano na vifaa vya upasuaji na mifuko ya kuhifadhia damu. Vifaa vingi hivi vya plastiki vimefanikiwa kutokana na maendeleo ya kemia. Hata nepi ambazo hutengenezwa maalumu kwa watoto hutumia kemikali maalum ili kuweza kukinga na athari za uvimbe ama maumivu makali yanayoweza kutokea katika ngozi nyepesi za watoto. Dawa za kuulia vijidudu na kuondosha madoa Kemia imeturahisishia katika kusafisha nyumba zetu, kusafisha na kutoa ukungu (kuvu) pamoja na madoa. Mwanzoni mwa miaka ya 1900, kemia ililenga zaidi katika kudhibiti bekteria, kusafisha nguo pamoja na nyumba zetu kwa uhakika. Katika mwaka 1913, tafiti ziliendelea zaidi kwa kugunduliwa kwa dawa ya kuondosha madoa ambayo pia ni rahisi kutumika. Sasa dawa ya kuondosha madoa imekuwa ni muhimu sana kwa matumizi ya nyumbani ambayo pia ni maarufu kwa kuulia vijidudu na hutukomeza kiwango kikubwa cha bekteria pamoja na vidudu vingine-ambukizi vya maradhi. Klorini (chlorine) pia ni silaha maradufu dhidi ya maradhi yanayosababishwa na virusi (viruses) pamoja na bekteria (bacteria) majumbani mwetu, hospitali pamoja na majengo mengine. Ignatius Semmelweis, mtaalamu wa Hungary wa magonjwa ya wanawake kwa mara ya kwanza alitumia maji yaliyochanganywa na klorini kwa kuosha mikono katika idara yake mnamo mwaka 1847.