1 / 19

Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam

Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam. 24 Mei 2006. Yaliyomo. Utabulisho wa UWABA Umuhimu wa njia za baisikeli Hali ya barabara za Dar es Salaam kwa wapanda baisikeli Mapendekezo yetu Vipi tunaweza kushirikiana kati ya UWABA na TANROADS . 1) Utambulisho wa UWABA.

Download Presentation

Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

  2. Yaliyomo • Utabulisho wa UWABA • Umuhimu wa njia za baisikeli • Hali ya barabara za Dar es Salaam kwa wapanda baisikeli • Mapendekezo yetu • Vipi tunaweza kushirikiana kati ya UWABA na TANROADS

  3. 1) Utambulisho wa UWABA • Umma wa Wapanda Baisikeli Dar es Salaam • Wanachama 50, wote wapanda baisikeli Tumeanzisha januari 2006 Tumesajili na serikali Tovuti: www.geocities.com/UwabaDar

  4. Utambulisho wa UWABA Malengo yetu: • Kushirikiana na serikali kutafuta mazingira mazuri na usalama kwa wapanda baisikeli Dar es Salaam • Kufuatilia haki za wapanda baisikeli • Kuelimisha wapanda baisikeli kuhusu matumizi mazuri ya barabara • Kuhamasisha watu kupanda baisikeli

  5. 2) Faida za baisikeli • zinaondoa msongamano wa magari • zinalinda mazingira • zinakuza uchumi • zinaboresha afya

  6. Umuhimu wa njia za baisikeli • Kupunguza msongamano wa magari • Wanafunzi kufika shuleni mapema • Kurahisisha watu kufika kazini na kufanya biashara • Kurahisisha kusafirisha bidhaa • Kurahisisha kuuza bidhaa (matunda, icecream) • Watu wa siyojiweza - walemavu, wagonjwa, wazee • Mazoezi na michezo

  7. Umuhimu wa njia za baisikeli • 37% za safari za Dar es Salaam ni kwa miguu au baisikeli • Mwaka 1994 wapanda baisikeli 24 na watembea kwa miguu 63 wamekufa na ajali Dar es Salaam, siku hizi zaidi • Tulipouliza kwa nini watu hawapandi baisikeli, 60% za majibu yalihusu usalama • Usalama unahusu sheria za barabarani, polisi na udereva lakini miundombinu ni muhimu zaidi

  8. 3) Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Morogoro Road • Kuna njia moja kwa wapanda baisikeli na watembea kwa miguu • Mijini – ni nyembamba, misingi ya barabara inasababisha waendesha baisikeli kushuka mara kwa mara. • Fire – teksi zinapaki njiani • Jangwani – karavat – lazima kushuka baisikeli mara nyingi kila upande. • Manzese na Ubungo wafanyabiashara wanaziba njia kabisa.

  9. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Kawawa Road • Njia moja baisikeli na watembea kwa miguu • Njia inapita mbele ya vituo vya mabasi siyo nyuma - ngumu kwa baisikeli kupita katika watu wengi wanaosubiri. • Kati ya Kigogo na Msimbazi njia ni embamba sana baisikeli haiwezi kupita • Teksi na lori zinanapaki njiani mfano Kona ya Bora • Kinondoni kuna wafanyabiashara wengi njiani wanaziba njia • Magomeni kuna nguzo zinaziba magari kuingia njiani - hii ni nzuri • Nyerere Road mpaka Kilwa Road, hakuna njia ya baisikeli wala watembea kwa miguu • Eneo la Keko, barabara ni nyembamba na watu wengi barabarani

  10. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Nyerere Road • Mijini –misingi, baisikeli inatumia njia ya magari • Kariakoo-Ilala njia nzuri sana upande mmoja, kuliko upande mwingine • Njia inapita nyuma ya kituo darajani - nzuri • Njia ya baisikeli lami ni tofauti na eneo la watembea kwa miguu lakini hakuna alama • Njia imeharibika sana karibu na Shoprite

  11. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Nelson Mandela Road • Sehemu nyingine kuna njia ya baisikeli na watu, sehemu nyingine hakuna kabisa (kama kati ya gereji na Mabibo External) • Sehemu nyingine njia ni ya vumbi, mashimo mengi, tupu na michanga mingi. Tabata shimo kubwa inalazimika kushuka. • Sehemu nyingi lori zinapaki njiani kama Vingunguti, Gereji, Mabibo External • Taxi zinapaki njiani – External na River side. • Corner Bar malori yamegeuza gereji njiani. • Tabata njia ni embamba sana baisikeli haiwezi kupita na mtembea kwa miguu • Riverside ngumu kupita kituo cha dala dala • Matawi ya miti yapo chini inazuia kuona pande zote za barabara-ajali ni nyingi • Karibu na Ubungo kuna wafanyabiashara wengi njiani

  12. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Kilwa Road, Mbande • Hakuna njia ya baisikeli kabisa na wapanda baisikeli wengi • Barabara ya magari nyembamba sana – magari hayawapi nafasi wapanda baisikeli • Mbande hakuna njia ya baisikeli kabisa • Mbande hakuna vituo vya mabasi maalumu

  13. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Ali Hassan Mwinyi • Njia moja- baisikeli na watembea kwa miguu • Vituo vya mabasi vya Aga Khan, Palm Beach watu wengi, ngumu kupita • Palm Beach teksi zinapaki njiani • Salanda Bridge, Kinondoni Road, Kenyatta Rd - misingi • Lami imeharibika sana kati ya Salandar Bridge na Ubalozi wa Ufaransa • Njia nzuri kati ya Ubalozi na Best Bite • Kati ya Best Bite na Morocco magari mengi yanapaki njiani yanaziba njia kabisa • Kutoka Morocco mpaka Regent ni pazuri ila ni nyembamba sana • Kutoka Regent mpaka Tegeta hakuna njia za baisikeli wala waenda kwa miguu. • Eneo la Sayansi taxi zinapaki njiani.

  14. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Sam Nujoma Road • Hakuna njia ya baisikeli wala watembea kwa miguu, hata sehemu ya vumbi ni mbovu • Darajani baisikeli haiwezi kupita njia ya pembeni kwa ajili ya nguzo, daraja mbovu na nyembamba • Hakuna vituo vya mabasi maalum, mabasi yanaziba njia yanaposimama

  15. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – New Bagamoyo Road • Kati ya Mwenge na Lugalo kuna njia upanda moja ila darajani kuna nguzo nyembamba sana baisikeli haiwezi kupita • Lugalo – Wazo: hakuna njia ya baisikeli wala waenda kwa miguu, barabara nyembamba

  16. Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Old Bagamoyo Road • Hakuna njia ya baisikeli wala watembea kwa miguu • Shoppers Plaza kuna msongamano sana wa watu na hakuna kituo cha mabasi maalum, nguma kupita • Barabara ya magari ni nyembamba magari yanapita baisikeli kwa karibu • Madaraja membamba • Maeneo ya Kawe watu wengi kituoni, ngumu kupita

  17. 4) Mapendekezo yetu • Njia hasa kwa baisikeli, njia hasa kwa watembea kwa miguu, sehemu maalum kwa wafanya biashara bila kuziba njia • Linda njia ya baisikeli kutoka magari – mfano karavat, kerbs, nguzo – epuka magari kuendesha na kupaki kwenye njia ya baisikeli • Njia na nguzo ziwe pana ya kutosha kwa guta na kwa baisikeli kupitana • Njiani uwezo wa kupita bila kushuka na kupanda tena (misingi njiani, mashimo makubwa, karavat njiani)

  18. Mapendekezo yetu • Njia ipite nyuma ya vituo vya dala dala • Alama kuonyesha njia ya baisikeli iko wapi • Drainage kuepuka maji mengi njiani • Mataa na reflectors • Sehemu za kuvuka barabara kwa watembea kwa miguu na wapanda baisikeli (U-turn, zebra) • Kama nafasi ipo, miti inayoleta kivuli bila kuziba njia

  19. 5) Ushirikiano UWABA tunapenda kushirikiana na TANROADS. Tunaweza kuwasaidia: • Kufanya savei za barabara • Kutoa maoni wakati wa kupanga, kujenga na kurekebisha barabara • Kutoa feedback kuhusu hali za barabara • Kuhamasisha watu kutumia barabara vizuri Tunapenda kuendelea kuwasiliana na kutana na TANROADS Dar es Salaam

More Related