1 / 2

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA

IV. CHAKULA NA KILIMO.

kiona
Download Presentation

MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA

An Image/Link below is provided (as is) to download presentation Download Policy: Content on the Website is provided to you AS IS for your information and personal use and may not be sold / licensed / shared on other websites without getting consent from its author. Content is provided to you AS IS for your information and personal use only. Download presentation by click this link. While downloading, if for some reason you are not able to download a presentation, the publisher may have deleted the file from their server. During download, if you can't get a presentation, the file might be deleted by the publisher.

E N D

Presentation Transcript


  1. IV. CHAKULA NA KILIMO Kemia na wahandisi kemia wametoa mchango mkubwa sana katika masuala ya chakula na kilimo kwa kuongeza uzalishaji zaidi wa mazao pamoja na matumizi ya vyakula vyenye virutubisho. Mwishoni mwa karne za 19 na 20 asilimia kubwa ya majiko yetu yalijaa mavuno ya vyakula kutoka katika ghala za kuhifadhia vyakula vya mizizi, bustani ama mashamba ya kienyeji; siagi iliyotengenezwa kutoka katika maziwa safi, mayai kutoka katika kuku waliofugwa upenuni, mboga kutoka katika bustani, nyama iliyohifadhiwa kutoka katika sanduku la barafu na kupikwa kwa mkaa wa mawe au kuni. Katika karne iliyopita tumeshuhudia mbadiliko makubwa sana juu ya namna ya kupata vyakula vyetu, uzalishaji zaidi katika mashamba yetu na urahisi wa kupatikana kwa vyakula pamoja na maji. Wakulima wa kisasa wameweza kutumia kemikali kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo. Matumizi ya mbolea na dawa za kuulia wadudu waharibifu wa mazao yamepelekea mavuno kupatikana kwa wingi na kwa uhakika zaidi. Jamii imefaidika na teknolojia mpya ambayo imechangia katika kuboresha ladha, umbo, upatikanaji wake pamoja na wingi wa virutubisho kutoka katika vyakula hivyo. Maendeleo na mafanikio haya katika kemia yamesaidia sana kulisha ulimwengu unaoendelea kwa kasi ya ongezeko la watu. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – MAONI YA WAKEMIA IV.1. Mbolea na Virutubisho vya Udongo Mbolea za Naitrojeni Mpango wa Haber-Bosch Ubora wa mbolea za kemikali Mapinduzi ya Kijani na mimea ya kupandishia (chotara) IV.2. Uhifadhi wa Mazao na Udhibiti wa wadudu waharibifu Mpango wa Bordeaux na dawa za kuondosha ukungu/kuvu DDT na dawa za kuulia wadudu Tiba/Uhifadhi wa wanyama Matunzo/Uhifadhi wa mashamba IV.3. Utengenezaji, Uhifadhi na Usalama wa vyakula Sakarini na Vikolezo utamu Vitamini na madini Hatua za uhifadhi na uzalishaji. Usalama wa vyakula na ubora wake IV.4. Uhifadhi wa Chakula Hifadhi katika vyakula Mafriji (jokofu) na kloroflorokaboni Majiko ya Maikrowevu Maji safi na salama

  2. IV. MATUKIO MUHIMU YA TEKNOLOJIA – CHAKULA NA KILIMO Louis Pasteur akidunga sindano wanyama. Matukio 1881Mwanasayansi wa Kifaransa Louis Pasteur agundua tiba ya kimeta kwa kondoo na nguruwe mwitu. 1883Mkemia wa Kidenish Johan Gustav Kjeldahl aboresha njia za kugundua kiwango cha naitrojeni katika vitu/mazao asilia. 1884Mwanasanysi wa Kifaransa Pierre M. A. Millardet agundua mchanganyo wa Bordeaux kupambana na kuvu/ukungu katika mashamba ya mizabibu. 1901John F. Quenny, mwanzilishi wa Kampuni ya Monsanto inayotengeneza Saccharin. 1913Wakemia wa Kijerumani, Fritz Haber na Carl Bosch waboresha uzalishaji wa kiwango kikubwa cha ammonia kwa matumizi ya viwandani. 1913Elmer V. McCollum na Marguerite David wagundua Vitamin A katika samli na kiini cha yai. 1918Kampuni ya Kelvinator yazindua kwa mara ya kwanza friji (jokofu) kwa matumizi ya kawaida. 1933Maziwa yenye viongezo vya Vitamin D yaanza kuuzwa. 1939Mwanakemia wa Uswissi Paul Mueller agundua matumizi ya DDT, dawa ya kuangamiza wadudu waharibifu. 1943Wanakemia wa Idara ya Kilimo nchini Marekani yazindua dawa ya kupuliza aerosol kwa kuua vijidudu na matumizi ya mashambani. 1953Saran wrap kwaajili ya matumizi ya kawaida yaanzishwa na kampuni ya Dow. 1964‘Mapinduzi ya Kijani’: Mpango wa mimea ya kupandishia (chotara) na matumizi ya mbolea za maji maji zimesaidia kuondosha tatizo la lishe kwa nchi. 1972Matumizi ya DDT yapigwa marufuku nchini Marekani (ikiwa nchi ya kwanza duniani, Hungary imepiga marufuku 1968). 1974Monsanto yagundua dawa ya kuua magugu. 1990 Usanii katika chakula kwa kuchanganya virutubisho vya lishe na chembe-chembe za madawa zaanza kupata umaarufu. Kipimo cha Kjelhahl cha kugundua kiwango cha naitrojeni katika vitu/mazao asilia Pierre M. A. Millardet Kiini cha yai chenye vitamin A Kasha asilia la Sakarini (Saccharin) Maziwa yakiwa na viongezo vya vitamin D Friji (jokofu) la kawaida la Kelvinator Bango-ujumbe la Monsanto Kasha asilia la kufungia DDT

More Related