360 likes | 579 Views
NGUVU NA UDHAIFU WA NGOs ZA KI-ISLAM TANZANIA. Mussa J ASSAD. STATEMENT OF DISCLAIMER. YALIYOMO NI MAONI BINAFSI. HAYAWAKILISHI TAASISI YEYOTE INAYOHUSIANA NAMI KATIKA JAMBO LOLOTE.
E N D
NGUVU NA UDHAIFU WA NGOs ZA KI-ISLAM TANZANIA Mussa J ASSAD
STATEMENT OF DISCLAIMER YALIYOMO NI MAONI BINAFSI. HAYAWAKILISHI TAASISI YEYOTE INAYOHUSIANA NAMI KATIKA JAMBO LOLOTE. NIA NJEMA NDIYO YENYE KUKUSUDIWA. MIFANO YA TAASISI IKITOKEA KUTAJWA BASI ICHUKULIWE KAMA MIFANO YA MAFUNZO TU NA SI TATHMINI KAMILIFU YA NAMNA TAASISI INAVYOFANYA VIZURI AMA VIBAYA. 16 September 2014 2
UTANGULIZI • . 16 September 2014 3
NGOs – NINI TAFSIRI YAKE? • NON GOVERNMENTAL ORGANISATIONS; • TAASISI MBADALA; TAFSIRI YA KINYUME – YENYE KUKANA – TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI; • KWANINI TAFSIRI YA KINYUME? • ZINAFANYA YALE AMBAYO SERIKALI INAYAFANYA BILA TIJA AU IMESHINDWA KUYAFANYA; 16 September 2014 4
‘CRUCIAL PILLAR OF INTERTANTIONAL HUMANITARIAN ARCHITECTURE’. 16 September 2014 5
HISTORIA FUPI YA NGOs • MAFUNGU MATATU YA KIHISTORIA [za-KIDINI, DUNANTIST na WILSONIAN]; • Za-KIDINI NI ZA ZAMANI KULIKO ZOTE NYINGINE [WAMISSIONARI WAKIANDAMA NA WAKOLONI] – HURUMA NA SADAKA; 16 September 2014 6
HISTORIA FUPI YA NGOs • NGOs za-KIDINI WAKATOLIKI WANAONGOZA KWA UKUBWA WA TAASISI NA MUONEKANO [VISIBILITY]; • CHRISTIAN REFUGEES SERVICES [CRS], CARITAS, CAFOD; • PROTESTANTS – WORLD VISION, etc 16 September 2014 7
HISTORIA FUPI YA NGOs • DUNANTIST – KUTOKANA NA HENRI DUNANT ALIEANZISHA RED CROSS KAMA MFUMO WA TAASISI YA KIBINADAMU KUKINGA RAIA KATIKA VITA; SAVE THE CHILDREN UK ILIANZISHWA WAKATI WA VITA KUU YA PILI KWA MTAZAMO WA DUNANT. OXFAM, nk. 16 September 2014 8
HISTORIA FUPI YA NGOs • WILSONIAN – KUTOKANA NA RAIS WOODROW WILSON WA MAREKANI; • LENGO NA TAMAA [AMBITION] – KUENEZA TASWIRA NZURI YA MISINGI YA MAISHA NA USHAWISHI WA MAREKANI KAMA NJIA NZURI YA KUFANYA WEMA KATIKA DUNIA; • CARE, PACT, nk. 16 September 2014 9
NGOs – MAENDELEO KARNE YA 20 • NGOs ZIMEONGEZEKA MARADUFU NUSU YA PILI YA KARNE YA 20 KATIKA MATAIFA YALIOENDELEA; • VIGOGO KATIKA NGOS – CARE, CRS, MSF, OXFAM, SAVE THE CHILDREN, WORLD VISION; • CARE, CRS, SAVE THE CHILDREN, WORLD VISION KWA PAMOJA WALIPEWA ROBO YA BAJETI YA MAREKANI YA MISAADA NA MAENDELEO. 16 September 2014 10
NGOs – MAENEO YA SHUGHULI • MISAADA YA DHARURA KATIKA MAJANGA [EMERGENCY RELIEF]; • REHABILITATION KWA MAANA YA UWEZESHAJI KURIDISHA MAISHA YA KAWAIDA BAADA YA MISUKOSUKO; NA • MAENDELEO [DEVELOPMENT]. 16 September 2014 11
NGOs – MAENEO YA SHUGHULI 16 September 2014 12
NGOs ZA KI-ISLAM • HAZIFAHAMIKI VIZURI AMA KWA UDHAIFU WAO AMA KWA UTASHI WA WENYE KUWEZESHA KUFAHAMIKA; • MPAKA MIAKA YA KARIBUNI HAZIKUWA ZINAINGIZWA KATIKA MAZUNGUMZO YA KIMAENDELEO [Development Discourse]; • LAKINI SASA ZIMEANZA KUONEKANA KAMA MHIMILI MUHIMU KATIKA KUWAENDEA WAISLAM [ISLAMIC RELIEF, MUSLIM AID, ETC.]. 16 September 2014 13
VITOFAUTISHI VY NGOs ZA KIISLAM • UISLAM KAMA ULIVYO DUNIANI SASA HIVI HAUNA MSONGE WA MADARAKA [Hierarchy]; • HAKUNA UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA KATI YA NGOs NA VIONGOZI WA DINI NA IBADA; • MATOKEO -> ADHOC EMERGENCE, KUKOSEKANA URATIBU [COORDINATION] NA KUUNGANA NGUVU KWA MAMBO YENYE MANUFAA YA PAMOJA KWA JAMII. 16 September 2014 14
VITOFAUTISHI VY NGOs ZA KIISLAM • SADAKA NA ZAKA NI SEHEMU YA DINI NA IBADA KATIKA UISLAM. DINI NYINGINE HAZIWEZI KUDAI JAMBO HILI KUTOKA MOJA KWA MOJA KWENYE MAANDIKO YAO; • HIVYO NI JAMBO LA LAZIMA KUTOA ZAKA NA INAKOKOTEZWA KUTOA SADAKA VILEVILE. NI JUKUMU LA WALIOJAALIWA KUWATAZAMA WALE AMBAO HAWAKUJAALIWA. SI JAMBO LA UTASHI TU, NI HAKI ZA WATU. 16 September 2014 15
MAENEO DHAIFU YA NGOs ZA KIISLAM STATEMENT OF DISCLAIMER NIA NJEMA NDIYO YENYE KUKUSUDIWA. MIFANO YA TAASISI IKITOKEA KUTAJWA BASI ICHUKULIWE KAMA MIFANO YA MAFUNZO TU NA SI TATHMINI KAMILIFU YA NAMNA TAASISI INAVYOFANYA VIZURI AMA VIBAYA. 16 September 2014 16
MAENEO YENYE NGUVU YA NGOs ZA KIISLAM • SADAKA NA ZAKA NI SEHEMU YA IBADA KATIKA UISLAM; • KWA SEHEMU KUBWA NGOs ZA KI-ISLAM HAZINA UBADHIRIFU WA DHAHIRI NA WENYE KUENDELEA UNAOONEKANA NDANI YA NGOs NYINGINE. KWANINI? • KUWAJIBIKA KWA ALLAH [SWT]; • WAISLAMU HAWANA STAHA NA ISRAFU JUU YA MALI YA SADAKA. MAKELELE YATAPIGWA NA HABARI KUFIKISHWA. 16 September 2014 17
MAENEO YENYE NGUVU YA NGOs ZA KIISLAM • IDADI YA WAUMINI NI KUBWA NA WANAKUTANA MARA NYINGI ZAIDI; • NAFASI KUBWA ZA KUSEMEA NA KUSIMAMIA MAMBO YAO IPO. INGAWA KUNA WASIWASI KWAMBA HATUSHUGHULIKI NAYO NAFASI HIYO; • NA KADHALIKA. 16 September 2014 18
MAENEO DHAIFU YA NGOs ZA KIISLAM KUBUNI, KUTEKELEZA NA KUSIMAMIA MIKAKATI • ‘THERE ARE NO BAD SOLDIERS, ONLY BAD GENERALS’ • MKAKATI NI KAZI MAHSUSI YA BODI YA WADHAMINI NA WAKURUGENZI PAMOJA NA MKUU WA TAASISI; • AGHALABU, HAKUNA MKAKATI WA TAASISI ULIYOFANYIWA KAZI INAYOSTAHILI; • UTEUZI WA BODI HAUTILII MAANANI UWEZO WA WATEULE BALI VITU VINGINE [???]. 16 September 2014 19
KUBUNI, KUTEKELEZA NA KUSIMAMIA MIKAKATI • MITAZAMO YA NGOs ZA KI-ISLAM IMEJIKITA ZAIDI SEHEMU MOJA – DAAWAH; • MISIKITI, MADRASAH, KUSOMA QURAN, KUCHAPISHA VITABU VYA DINI NA KUGAWA BURE AU KWA BEI YA CHINI, NK. • JE VIPI MAZINGIRA? HAIPO SEHEMU YAKE KATIKA UISLAMU? KUONGEZA KIPATO CHA WAISLAMU? VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA? NK. ZIPO JUHUDI LAKINI KIDOGO SANA. TUNAHITAJI WIGO MPANA ZAIDI, PAMOJA NA UDHAIFU WETU. 16 September 2014 20
MAENEO DHAIFU YA NGOs ZA KIISLAM UONGOZI NA UENDESHAJI WA TAASISI • ‘US NGOs have a strong corporate model’ • PROFESSIONALISM INAHUSIANA SANA NA ORGANISATIONAL EFFECTIVENESS. SASA JE TUNAONAJE WELEDI WA TAASISI ZETU NA UBORA WA UTENDAJI WAKE? • TAFITI ZINAONYESHA KWAMBA NGOs NYINGI ZINA TATIZO ENEO HILI. JE ZA KI-ISLAM? 16 September 2014 21
UONGOZI NA UENDESHAJI WA TAASISI [2] • NGOs ZA KI-ISLAM HAZITABIRIKI MTAZAMO WAKE KWA KUTEGEMEA IMANI YA UISLAM PEKE YAKE BALI PIA HUTEGEMEA TAFSIRI NA MITAZAMO TOFAUTI YA VIONGOZI WAKE. NAYO HII HUTOKANA NA TAMADUNI NA MIFUMO YA ELIMU WALIOSOMEA VIONGOZI WA TAASISI; • ATHARI YAKE NI MAHUSIANO YA JUU JUU NDANI YA NCHI NA ‘SUFURI’ NJE YA NCHI. 16 September 2014 22
UONGOZI NA UENDESHAJI WA TAASISI [2] • NGOs ZA KI-ISLAM HAZIONGOZWI KATIKA MISINGI SAHIHI YA UADILIFU WA VIONGOZI – YAANI KIONGOZI KUWA WAKATI WOTE NA RADHI ZA ANAOWAONGOZA; • FOUNDER’S SYNDROME, BABA, BABU, ETC. 16 September 2014 23
UONGOZI NA UENDESHAJI WA TAASISI [2] • VIONGOZI WANAOIJUA DINI SI LAZIMA WAWE VIONGOZI WA TAASISI KAMA NGOs – WATAFUTWE VIONGOZI WENYE SIFA ZINAZOTAKIWA KUKIDHI MAHITAJI; • ATHARI YAKE NI UGOMVI, KESI NA MUDA MWINGI VIONGOZI KUTUMIA KUTETEA NAFASI ZAO BADALA YA KUFANYA KAZI ZA KUPELEKA MBELE TAASISI. 16 September 2014 24
MAMBO YAHUSUYO IDENTITY [UTAMBULISHO NAFSI] • NGOs ZA KI-ISLAM ZINAJITAMBULISHA MOJA KWA MOJA NA IMANI YA DINI YA KI-ISLAM KAMA NGUVU YA MSINGI YA UHAI WA TAASISI. HILI NI JAMBO ZURI SANA LAKINI LINA GHARAMA ZAKE. TURKISH MUSLIM NGOs ZIMEJITOFAUTISHA KIDOGO KATIKA HILI. JE LINAFAA JAMBO HILI KATIKA MAENEO FULANI FULANI? HOUSING COOPERATIVE, KWA MFANO. 16 September 2014 25
MATATIZO YA MIFUMO YA UENDESHAJI • KWA UJUMLA WAKE MIFUMO YA UENDESHAJI, HATUSEMI MIBAYA, LAKINI INAHITAJI KUWA MIZURI ZAIDI; • VITU GANI? – MAHUSIANO YA NAFASI [STRUCTURE], MAWASILIANO YA NDANI NA NJE, MIKUTANO NA USHIRIKI KATIKA NGAZI ZOTE, UWEKAJI NA UTUNZAJI WA TAARIFA NA KUMBUKUMBU, UCHAPISHAJI NA UTOAJI WA TAARIFA ZINAZOFAA NA ZINAZOTAKIWA, ETC. 16 September 2014 26
MATATIZO YA MIFUMO YA UENDESHAJI • UDHAIFU WA WAISLAM WENYE UJUZI KILA MMOJA WAO KWA KIWANGO CHAKE KWA KUSHINDWA KUSAIDIA KWA JUHUDI ZAKE ZOTE KATIKA MAENEO ANAYOWEZA KUSAIDIA; • COMPETENCIES ARE EVIDENT WHERE WE WORK FOR OUR EMPLOYERS [for money] BUT NOT IN OUR MUSLIM NGOs! • LABDA NGOs ZETU NDOGO NDOGO MNO LAKINI NDIZO ZINAZOHITAJI UWEZO WA MIFUMO MIZURI ZAIDI. 16 September 2014 27
UPUNGUFU WA WAFANYAKAZI WAENDESHAJI • JE TUNA KUNDI [POOL] LA WAFANYAKAZI TUNAOWEZA KUWATUMIA IKILINGANISHWA NA NGOs NYINGINE? • JE KUNA MFUMO WA KUWAENDELEZA KUWA ‘DEVELOPMENT PROFESSIONALS’ WALE TULIONAO? NA JE NI MUHIMU KWELI JAMBO HILI? • PART TIME/WEEK-END DEVELOPMENT PROFESSIONALS? 16 September 2014 28
WASAA MDOGO UMEACHWA KWA MAMA NA DADA ZETU • SI HABARI YA MAZUNGUMZO YA KILEO NA POLITICAL CORRECTNESS. HILI NI JAMBO MUHIMU SANA; • TAZAMA NA FUATILIA KURA ZA MAONI PALE KINA MAMA WALIPOWEKA MSIMAMO WAO; • NETWORKS ZA KINA MAMA NI INTENSIVE, STRONGER AND BIGGER; • HATUNA FURSA YA KUACHA KUWAHUSISHA KIKAMILIFU. 16 September 2014 29
UTOAJI DHAIFU NA WA MSIMU • UTOAJI DHAIFU NA WA MSIMU UNA ATHARI HIYO HIYO KWENYE TAASISI; • ZAKA NA SADAKA MARA NYINGI HUTOLOWA WAKATI WA MFUNGO WA RAMADHANI. LAKINI MAHITAJI YA WAISLAM WENYE DHIKI NA MAISHA DUNI YAPO MWAKA MZIMA! • UTOAJI UNAFUNGWA KATIKA MAENEO MACHACHE YENYE ‘BIMA ZA THAWABU’ [MISIKITI, MADRASA, KUHIFADHI QURAN, ETC]. 16 September 2014 30
HABARI YA FEDHA • UISLAM UNAPENDELEA ZAIDI SIRI KATIKA UTOAJI WA SADAKA. HIVYO WATOAJI HAWATAKI KUFAHAMIKA. KATIKA MAENEO YENYE MIFUMO MIBOVU YA UTENDAJI HILI JAMBO HULETA FITNA KUBWA; • KITU GANI KIMEPOKEWA NA NANI, NA KIMETUMIKA NAMNA GANI? INAWEZEKANA SIRI YA UTOAJI KUTUNZWA NA BADO KUMBUKUMBU NZURI ZIKAWEKWA NA KUCHAPISHWA. 16 September 2014 31
NYONGEZA JUU YA HABARI YA FEDHA • KUTOKANA NA HILI LA FITNA YA FEDHA WATOAJI WANATAZAMA NANI MTU ANAYEAMINIKA [si TAASISI] AMBAYE ATAWEZA KUSIMAMIA AMANA YA FEDHA NA VITU KAMA HIVYO; • HAWA SASA WANAKUWA WATU MUHIMU KAMA VIUNGANISHI INAPOTOKEA TAASISI ZINAHITAJI UWEZO WA KIFEDHA KUTEKELEZA MAJUKUMU; • WAFADHILI WA NJE? INAKUWA TAABU. 16 September 2014 32
NYONGEZA JUU YA HABARI YA FEDHA • BAADA YA 9/11 WATOAJI WANAPATA MISUKOSUKO KWANI NGOs ZA KI-ISLAM ZINASHABIHISHWA NA UGAIDI, PALE STICKER HII INAPOONEKANA INAFAA. LABDA TUWEKE NA KUBAINISHA HABARI ZETU ZA FEDHA DHAHIRI HASA KWA WASHIKADAU WETU. KAMA TUNAVYOFANYA KATIKA BAADHI YA MISIKITI YETU. 16 September 2014 33
MANENO YA KUMALIZIA • ‘IT IS NOT ALL DOOM AND GLOOM – LOTS OF BRIGHT SPOTS’ • TUZIJENGEE UWEZO NGOs ZETU KATIKA NAMNA AMBAYO TUTAPATA KUONGEZA UAMINIFU WA WATU, VIONGOZI NA TAASISI. LAKINI PIA UWEZO UTATUONGEZEA HESHIMA JUU YA TAASISI ZETU, HASA KATIKA MASHIRIKIANO NA TAASISI NYINGINE NDANI NA NJE YA NCHI; • IPO NAFASI NA DHIMA KUBWA KWA ‘MUSLIM PROFESSIONALS’ KUSAIDIA. 16 September 2014 34