110 likes | 263 Views
CHANGAMOTO NA MAONI YA NSAs. MEDIUM TERM EXPENDITURE FRAMEWORK AND CROSS CLUSTER STARTEGY.
E N D
CHANGAMOTO NA MAONI YA NSAs MEDIUM TERM EXPENDITURE FRAMEWORK AND CROSS CLUSTER STARTEGY
Sehemu 11: kutokana na mtikisiko wa uchumi katika dunia uchumi wa Tanzania unategemewa kupungua kwa 7.3% katika mwaka 2009( hali hii inajichanganya na kauli za viongozi na wataalamu mbalimbali wa serikali amabao wanasema kuwa hali hii haina madhara /kishindo kwa uchumi wa TZ)
Sehemu 13: Serikali imejizatiti kutimiza masharti ya mikopo na pia kuwezesha shughuli za MKUKUTA kikamilifu na kuwalipa vizuri watumishi wake ili watoe huduma zenye ufanisi. - Hali halisi ni kwamba sekta muhimu kama kilimo bajeti yake bado haitoshi. Serikali katika mkutano wa Maputo (2003) iliahidi kuongeza bajeti ya kilimo hadi 10% kufikia 2008. Bajeti ya 2008/2009 ni 6.2% ( tofauti 3.8)
Pamoja na juhudi ya kuongeza mishahara ya watumishi ili watoe huduma zenye ufanisi , hata hivyo huduma hizi bado hazitakuwa za kutosha kutokana na uchache wa watumishi hasa katika maeneo ya vijijini. • Huduma bora na yenye ufanisi haitapatikana kwa kuboresha mishahara tu , bado kuna haja kubwa ya kujenga uwezo wa watendaji
Sehemu 14: Inasadikika kuwa kipato cha Mtanzania kwa mwaka ni USD 500 amabacho kwa kiasi kikubwa kiko chini ya mategemeo ya vision 2025 ambacho ni USD 3,600: • Vigezo vinavyotumika katika kukokotoa per capita( kipato kwa mwaka ) si halisia kutokana na udhaifu wa ukusanyaji wa takwimu. Takwimu zetu nyingi hazina ubora. • Hali ya kipato na hali ya umasikini inaweza kuelezwa vizuri zaidi na watu wahusika ( walengwa) kuliko watu wa nje.
Sehemu ya 16: Inaeleza kuwa kuna maendeleo mazuri katika shule za msingi na sekondari hasa katika kujiandikisha na mahudhurio: - Vigezo vya kupima maendeleo katika elimu ni kujiandikisha kwa wingi ( quantitative enrolment) na mahudhurio ( attendance)? • Jambo la ubora wa elimu ni msingi zaidi kama tunataka kutekeleza vema MKUKUTA • Umiliki wa simu katika kaya unaweza kuchukuliwa kama kigezo cha kukua kwa uchumi , lakini kama taifa changa linaloendelea haliwezi kuwaeleza watu wa kawaida kama kitu cha kujivunia. Swali simu hizi ni za thamani gani, nani alinunua? Nani anwezesha kuziendesha?
Sehemu ya 34: Serikali inafuatilia matumizi ya MKUKUTA kwa kutumia ( IFMS) : - AZISE mbalimbali zimekuwa zikijihusisha na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma ( PETS) . Taarifa hizi zinatumikaje na serikali ili kuweza kupima thamani ya fedha ( Value for money)
Sehemu ya 60: Serikali inakiri kuwa na mapungufu katika kutoa fedha/ bajeti ya maendeleo kwenye wilaya na sekta mbambali: - Uko upungufu katika utekelezaji wa mipango ya DADPs sababu zikiwa ni za uchelewaji wa fedha kutoka serikali kuu . Iko haja ya kurekebisha utoaji wa bajeti has katika miradi ya kilimo inayendana na msimu.
HITIMISHO : • Kutokana na uwasilishi wa Paper hii ( MEDIUM TERM EXPENDITURE FRAMEWORK AND CROSS CLUSTER STRATEGY) inaonyesha dhahiri kuwa serikali imedhamiria kuutekeleza MKUKUTA kwa nguvu zote. Hata hivyo yafuatayo yanashauriwa: • NSAs zipewe/ wapewe nafasi zaidi ya kushiriki katika mchakato mzima wa kutengeneza bajeti na pia kwenye kutathimini • Bajeti izingatie zaidi mahitaji ya wananchi katika ngazi ya chini • Halmashauri zijengewe uwezo ili kuweza kusimamia bajeti kikamilifu
ANGALIZO: - TANZANIA SI MASIKINI KAMA INAVYODHANIWA . JAMBO LA MUHIMU NI KUZINGATIA UTAWALA BORA .