130 likes | 383 Views
Watawa wa St. Benet de Montserrat. PASAKA. ALELUYA!!!. ALELUYA!!!. ALELUYA!!!. Wimbo: Aleluya ya Hendel. Ni PASAKA. Tufurahini. Kanisa ya Yerusalemu ambalo inaaminika Kristu Yesu alifufuka. Picha ambazo ziko hapa ni za Basilika la Montserrat Catalonia- Spain mpigaji J.M. Subirachs.
E N D
Watawa wa St. Benet de Montserrat PASAKA ALELUYA!!! ALELUYA!!! ALELUYA!!! Wimbo: Aleluya ya Hendel
Ni PASAKA Tufurahini
Kanisa ya Yerusalemu ambalo inaaminika Kristu Yesu alifufuka
Picha ambazo ziko hapa ni za Basilika la Montserrat Catalonia- Spain mpigaji J.M. Subirachs
Jn 20:1-9 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi. Yule mwanafunzi mwenye imani, Maria Magdalena alikuwa wa KWANZA kufika kaburini ile alfajiri, iwapo MIMI, nilikuwepo macho yake bado hayakuwa tayari kushuhudia MAISHA MAPYA
Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, "Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka." Alikwenda mbio kuifaamisha KANISA, kwamba bado hamkuwepo NA ZAWADI YA PASAKA
Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine wakaenda kaburini. Wote wawili walikimbia lakini yule mwanafunzi mwingine alikimbia mbio zaidi kuliko Petro, akatangulia kufika kaburini. Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani. Yohane alimtangulia Petro kufika kaburini lakini Petro, ndiye alishuhudia wa kwanza fumbo la ufufuko
Simoni Petro naye akaja akimfuata, akaingia kaburini; humo akaona sanda, na kile kitambaa alichofungwa Yesu kichwani. Hicho kitambaa hakikuwekwa pamoja na hiyo sanda, bali kilikuwa kimekunjwa na kuwekwa mahali peke yake. Kitambaa kile kilionyesha kuwa Mwili wangu MTUKUFU ulipenyea juu yake bila kukiguza... Je inaweza kueleweka?
Kisha yule mwanafunzi mwingine aliyemtangulia kufika kaburini, akaingia pia ndani, akaona, akaaamini. Yule mwanafunzi niliyempenda alipoona hayo yote ALINIAMINI
Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka wafu. Maisha yangu sasa mbele ya wanadamu ni tofauti wale tu wanao IMANI ndio wanaweza kuyaelewa. Ama kweli nawaambia niko karibu nenyu ikiwa tu mnao UPENDO
Pasaka ni Mwangaza wa MILELE Kwa wote ambao wanamwamini Yesu mwana wa Mungu
Ewe Yesu mwema, kwa ufufuko wako umetupa MAISHA YA MILELE, geuza njia zetu ili wote ambao wanaotujogea washudie kwamba kweli tumepokea kipaji cha PASAKA
www.benedictinescat.com Imetayarishwa na: Regina MbithiKwa maoni, mawazo ama mawaidhausisite tuma kwa: regmbithi@yahoo.com