210 likes | 474 Views
KONDOMU. Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania. Historia ya Kondomu. Imetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania. Kondomu ni nini?. Kondomu Ni kama mfuko uliotengenezwa kwa kutumia mpira,plastiki au ngozi za wanyama
E N D
KONDOMU Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania.
Historia ya Kondomu Imetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania
Kondomu ni nini? Kondomu • Ni kama mfuko uliotengenezwa kwa kutumia mpira,plastiki au ngozi za wanyama • Inahifadhi mbegu za kiume kabla, wakati na baada ya mwanaume kukojoa • Ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango na pia ni kinga dhidi ya kuzuia magonjwa ya zinaa pamoja na virusi vya Ukimwi (VVU) • huepusha uume kuguswa na maji maji yatokayo ukeni.
Historia ya Kondomu.. • Kondom zinaweza kufuatiliwa takribani miaka elfu iliyopita… • Ushahidi wa kwanza unarudi kwa Wamisri!! • Katika miaka ya 1000 KK, walitumia mpira laini kujikinga kutokana na magonjwa ya zinaa…
Na wapi tena kwingine? • Michoro ya mapangoni iliyopo cambarelles nchini Ufaransa inaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka ya 100-200 BK kulikuwa na matumizi ya kondomu.
Malighafi gani ilitumika kutengeneza kondomu? • Kondomu hizi zilitengezwa kwa malighafi isiyo kawaida: • Mafuta ya hariri • Karatasi • Tumbo la samaki • Gamba la kobe
Mabadiliko ya kondomu • Kuna kipindi kondomu zilifungwa na kamba nyembamba..
Zatumiwa kama kinga dhidi ya maradhi - miaka ya 1500 • Janga la Kaswende lasambaa Ulaya… • Muitaliano, Gabrielle Fallopius, anajitangaza kutengeza kondomu ili kuwakinga wanaume kutokana na ugonjwa huo • Alifanya majaribio miongoni mwa wanaume 1,100 kutumia kondomu, hakuna anayeambukizwa kaswende.
Mabadiliko ya kondomu • Baadaye katika miaka ya 1500.. ufanisi wa matumizi ya kondomu katika kuzuia mimba unagundulika. • Kondomu zinarekebishwa: • Mifuko ya kitambaa ililowekwa kwenye kemikali na kuruhusiwa kukauka kabla ya matumizi. • Zilikuwa kondomu za kwanza zenye kemikali ya kuua mbegu za kiume.
Mabadiliko ya kondomu • Katika miaka ya 1700, uwenzo wa kondomu katika uzazi wa mpango unaanza kufahamika. • Kondomu zinazotengenezwa kwa utumbo wa wanyama zinaanza kuwepo. • Kondomu za aina hii zinajulikana na kuongezeka umaarufu.
Mabadiliko ya kondomu Miaka ya 1800, • Utengenezaji wa kondomu unabadilika baaada ya kugundulika maarifa ya kuchemsha malighafi ya mpira na sulphur ili kuifanya iwe mpira imara na unaonyumbulika. • Hii iliwezesha kutengeneza bidhaa za mpira zikiwamo kondomu, haraka na kwa bei nafuu. • Matokeo yake,matumizi ya kondomu yanaongezeka
Mabadiliko ya kondomu Miaka ya 1900 • Mpaka mapema miaka ya 1900 • kondomu nyingi zilitengenezwa kwa kuchovya mikono kwenye mchanyato wa mpira. • ubora wake haukuwa thabiti
Mabadiliko ya kondomu Mwaka 1919, • Fredrick Killian alianzisha uchovyaji kwenye mpira laini. • Kondomu za mpira zilikuwa bora kwani zilidumu kwa muda mrefu zaidi, nyembamba na hazikuwa na harufu.
Historia ya Kondomu • Katikati ya miaka ya 1930, watengenezaji wakubwa nchini Marekani walikuwa wakitengeneza kondomu milioni 1.5 kwa siku. • 1950: Ubora wa uhakiki, majiribio ya kwanza ya kondomu, kwa elekroniki yaanza. • Mwaka 1957, kondomu ya kwanza yenye kilainishi yazinduliwa Uingereza.
Historia ya Kondomu • Mwaka 1974 Dawa ya kuua mbegu za kiume ilianza kuwekwa kwenye kondomu. • Mwaka1994 kondomu za kiume zilizotengenezwa kwa plastiki (polyurethane) ziliingizwa kwenye soko.
Historia ya kondomu Tanzania • Baada ya vita kuu ya pili ya dunia, veterani walilete kondomu za kwanza nchini. • Mwanzo wa miaka ya 70,kondomu zililetwa kwa ajili ya kupanga uzazi na UMATI. • Utumiaji uliongezeka miaka ya 1980 baada ya janga la UKIMWI.
KONDOMU ZINAZOPATIKANA TANZANIA. • Kondomu za kiume zinazopatikana Tanzania zinatengenezwa kutokana na mpira laini. • Kondomu za kike zinazopatikana (kiasi kidogo) zinatengezwa na malighafi ya plastiki.
Usambazaji wa kondomu Tanzania Mwaka 2003, • Jumla ya kondomu 48.5 milioni zilisambazwa na mtandao wa vyombo vya kibiashara na kijamii