230 likes | 414 Views
KONDOMU. Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania. Kondomu Ulimwenguni. Kitini hiki kimetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania. Je Unajua kwamba…. Takribani Kondomu bilioni tisa zinasambazwa duniani kila mwaka!
E N D
KONDOMU Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania.
Kondomu Ulimwenguni Kitini hiki kimetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania
Je Unajua kwamba… • Takribani Kondomu bilioni tisa zinasambazwa duniani kila mwaka! • Hebu tuangalie nani hasa ni mtumiaji wa Kondomu ulimwenguni!
Utangulizi • Matumizi ya Kondomu Ulimwenguni yanatofautiana baina ya bara ana bara na hata baina ya nchi na nchi. … • Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 5 (tano)ya wanandoa walio katika umri wa kuzaa hutumia Kondomu… • Hata hivyo katika nchi nyingine zaidi ya asilimia 10 (kumi) ya wanandoa hutegemea zaidi Kondomu!!!
Tuangalie Takwimu chache... • Takribani wanandoa milioni 44 hutumia Kondomu kupanga uzazi! • Zifuatayo ni takwimu zinayoonyesha wanawake walio katika umri wa kuzaa na walitumia kondomu kama njia ya kupanga uzazi (2003): • Mauritania 13.3% • Botswana 11.2% • Korea ya kusini 15.1% • Singapore 22.0% • Tanzania 2.7%
Takwimu… • Kwa wenzi ambao hawajaoa au kuolewa matumizi ya Kondomu ni makubwa zaidi! • Latvia: Zaidi ya theluthi mbili wanatumia Kondomu! • Mexico: Wanaume 63% (1997) • Paraguay: Wanawake 79% (1996)
Matumizi ya Kondomu nchini Ujerumani • Mwaka 2002, Kondomu zipatazo milioni 201 zilisambazwa. • Theluthi mbili ya vijana hutumia Kondomu katika tendo lao la kwanza la kujamiiana! • Kondomu na vidonge vya uzazi wampango ni njia zinazotumiwa sana kwa ajili ya kupanga uzazi.
Ujerumani • Katika Ujerumani jamii imezikubali Kondomu. • Kampeni ya karibuni ilijulikana kama “USIUPATIE UKIMWI NAFASI” • Kampeni hii imeonyesha mafanikio makubwa, na inakadriwa kuwa takribani watu wapatao 25.000 walikingwa dhidi ya uambukizo mpya.
Uholanzi • Katika nchi hii vijana wanapata taarifa mbalimbali zinazohusiana na elimu ya afya ya uzazi na mahusiano ya kijinsia.
Uholanzi • Vijana na matumizi ya njia za uzazi wa mpango: Katika mwaka 2000: • 68 % walitumia kondomu • 27% walitumia kondomu na vidonge vya uzazi wa mpango. • 31% walitumia kondomu lakini si mara zote. • 17% Hawakutumia kondomu.
Japan… • Wajapani wana historia ndefu katika matumizi ya Kondomu…. • Waliweza kugundua kondomu waliyoiita 'Kawagata' au 'Kyotai‘ ambazo zilitengenezwa kutokana na ngozi nyembamba na 'Kabutogata‘ iliyotengenezwa kutokana na gamba la kobe au pembe.
Japan… • Jamii katika nchi hii inaikubali sana kondomu,hivyo kama kuna unyanyapaa kuhusu kondomu basi ni kidogo sana. • Pia , katika nchi hii kuna sheria inayozuia matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango, ambayo ilitungwa miaka 30 iliyopita.
Japan • Karibu asilimia 20 ya wanandoa wanaotumia kondomu ulimwenguni wanapatika Japan. • 46% ya wenza ,au 78% ya watu wote wanaotumia njia za uzazi wa mpango, wanategemea kondomu.
China • Serikali ya China inahamasisha matumizi ya uzazi wa mpango, ikizingatia mwongozo unaowataka wananchi kuzaa mtoto mmoja ili kudhibiti ongezeko la watu. • Hivyo basi, katika nchi hii wenza wengi hutumia kondomu kila mara.
Thailand • Katika miaka ya 1980 UKIMWI, ulichukuliwa kama ugonjwa wa wageni. • Lakini hali haikuendelea kubakia hivyo kwani, katika miaka ya 1990, idadi ya walioambukizwa ilifikia 300,000, kutoka hapo UKIMWI ukatangazwa kuwa janga la taifa.Hii ilifuatiwa na kampeni kubwa zilizozinduliwa na wizara ya afya ya nchi hii.
Thailand • Katika jitihada za kudhibiti UKIMWI, nchi hii ilitunga sheria ambapo watu wanao husika na biashara ya kuuza miili pamoja na wateja wao walitakiwa kutumia kondomu ‘ programu ya matumizi ya kondomu kwa asilimia 100. • Programu hii ilipata utashi mkubwa kutoka kwa wadau wote ikiwemo serikali na jamii nzima kwa ujumla
Thailand • Matumizi ya kondomu katika majumba ya biashara za ngono yalipanda kutoka 14% mwaka 1988 mpaka 95% mwaka 1995. • Takwimu za mwaka 2002 zinaonyesha kuwa maambukizi mapya yameshuka kwa zaidi ya asilimia 80%!
Uhamasishaji wa matumizi ya Kondomu • Uhamasishaji wa matumizi ya Kondomu unafanyika duniani kote, ukilenga katika kuzuia maambikizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana ( VVU na magonjwa mengine ya ngono) na mimba zisizotarajiwa.
Hitimisho • Kondomu zinatumiwa ulimwenguni pote! • …Yaani mabara yote matano!!!!!