230 likes | 468 Views
KONDOMU. Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania. Uhakiki wa ubora wa kondomu. Kitini hiki kimetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ,TBS na PSI-Tanzania. Kwanini uhakiki wa ubora ni muhimu. Umuhimu wa ubora: Katika kuzuia mimba zisizotarajiwa
E N D
KONDOMU Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania.
Uhakiki wa ubora wa kondomu Kitini hiki kimetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ,TBS na PSI-Tanzania
Kwanini uhakiki wa ubora ni muhimu • Umuhimu wa ubora: • Katika kuzuia mimba zisizotarajiwa • Katika kukinga dhidi ya magonjwa ya Ngono • Ubora usio wa uhakika huwafanya watumiaji kuwa na wasiwasi kuhusu kondomu na matumizi yake, hii inaweza kupunguza matumizi na kusababisha maambukizo.
Utangulizi • Mambo yafuatayo hufanyika ili kuhakiki ubora wa Kondomu… • Viwango vya Kimataifa vinavyoongoza utengenezaji wa Kondomu za kiume: • Ukaguzi wa Viwanda kuona kama vinaouwezo wa kutengeneza Kondomu zenye ubora unakubalika. • Ukaguzi na uhakiki wa ubora wa Kondomu kabla hazijatoka kiwandani.
Kondomu bora ni zipi? • Inabidi kuenea kwenye uume sawa sawa • Isiwe na matundu • Iwe na nguvu tosha • Imefungwa vizuri ili kuzilinda katika utunzaji • Imewekwa lebo sahihi
Kondomu bora ni zipi? • Kondomu, bidhaa ya kufungia na unga haitakiwi kuwa; • sumu • inayowasha • inayodhuru • Vipimo vya ISO 10993 huzingatia usalama.
Upimaji hufanyika lini? • Kwenye eneo makusanyo ya malighafi (mpira) • Wakati na baada ya utengenezaji na wenye viwanda. • Na mnunuzi
Tunathibitishaje ubora? • Hakiki bidhaa tayari: • Msambazaji anamtaarifu mnunuzi mzigo unapokuwa tayari kwa kusafirisha • Mnunuzi hupeleka baadhi ya bidhaa, toka kwenye kila mzigo, kwenye maabara kwa ajili ya vipimo vya kitaalamu
Tunathibitishaje ubora? • Kupima mzigo kwa mzigo:Kwa kutumia majedwali ya kupimia • Imechapishwa na International Organization for Standardization (ISO 2859-1) • Huhakiki ubora wa kitakwimu, ambao huwakilisha mzigo wote.
Tunathibitishaje ubora? • Mnunuzi anapata ripoti ya maabara: • Iwapo matokeo ya vipimo yanathibitisha ubora, mnunuzi humtaarifu mtengenezaji asafirishe kondomu. • Iwapo matokeo hayakubaliki, mnunuzi humtaarifu mtengenezaji kuharibu kondomu.
Upimaji maabara hufanyika vipi? • ISO 4074:2002 – Mahitaji na namna za upimaji: • Nguvu na ujazo wa kupasuka • Uimara na maisha • Kutokuwa na vitundu au kasoro • Uimara wa ufungaji (kutoingiza hewa,kutokuingiza vijidudu, kufungwa kwa uhakika) • Uwekaji lebo.
Kupima: Vipeo • Kupima urefu, kondomu hutanuliwa kidogo (mpaka asilimia 10) • Upana hupimwa nyuzi 90 kuangalia urefu wa kondomu. • Vipimo vitatu vya unene/wembamba hufanywa kwa kila kondomu
Kupima: “Uhuru wa kutokuwa na vitundu" • Katika njia ya kutundika, kondomu hujazwa maji • Mtaalamu hutazama kuona kama kuna yanapenya
Kupima: Uvujaji“Uhuru wa kutokuwa na vitundu • Njia ya kutundika/kutandaza • Mwisho unafungwa na kondomu inatandazwa kwenye karatasi ili kuangalia alama za maji kwenye karatasi • Pia izingatiwe kuwa Kondomu inaweza kujazwa lita 20 za maji bila kutetereka.
Kipimo: Tansila. • Kipande cha mpira chenye upana wa milimeta 20 hukatwa toka eneo la kati la kondomu • Katika Kupima, kipande hiki huvutwa hadi kukatika • Kipimo hupima • Nguvu itumikayo kupasua ule mpira • Urefu wa kipande cha mpira kinachopasuka • Nguvu itumikayo kukata ule mpira.
Kipimo: Mpasuko wa hewa • Kondomu hujazwa hewa kama puto • Kisha ujazo wa hewa na hewa inayosababisha kupasuka hupimwa
Kipimo: Ufungaji imara • Kondomu iliyofungwa huwekwa kwenye chumba kisicho na hewa • Iwapo itawekwa kwenye maji, baada ya dakika moja ya kutopata hewa, mapovu hutokea iwapo kuna vitundu • Iwapo itawekwa mahala pakavu na pasipo na hewa kwa dakika moja, kondomu hutakiwa kubaki bila hewa ili kipimo kiwe sahihi.
Kipimo: Kiasi cha mafuta • Kuhakiki kiasi cha kilainishi kwenye kondom iliyowekwa kilainishi, • Kipimo hiki hupima uzito wa • Kondomu iliyofungwa, • Kondomu yenye kilainishi, • Kilanishi kwenye kondomu, • Kilainishi kwenye mfuko, • Kondomu iliyosafishwa na mfuko uliosafishwa.
Kipimo: Kipimo cha Joto (oven) • Huonyesha bidhaa itakuwa thabiti kwa muda gani baada ya kuhifadhiwa • Kipimo hiki huifanya Kondomu iwe kama imekaa muda mrefu (imezeeka) • Baada ya hapa Nguvu itumikayo kukata na kupasua mpira hupimwa tena. • Matokeo hulinganishwa na taarifa nyingine.
Nani anafanya vipimo vya maabara? • Shirika La Viwango (TBS) hupima kondomu zote zizosambawa na kuuzwa Tanzania. • Ina vifaa vya kisasa kabisa, hivyo hutimiza viwango vya kimataifa. • TBS inafanya kazi hii kwa uaminifu:
Vipimo vina gharama gani? • Ni asilimia sita mpaka kumi (6-10%) ya gharama za ununuzi. • Vipimo ni muhimu kuhakikisha kuwa kondomu zina ubora unaokubalika • - kwahiyo, ni gharama muhimu!!!
Utunzaji na usambazaji • Kondomu hazitakiwi kutunzwa sehemu zenye joto kali, juani au unyevu. • Utafiti umeonyesha kuwa kondomu bora zilizofungwa sawa sawa haziharibiki kwenye nchi za tropiki
Hitimisho • Uhakiki wa ubora hufanyika wakati wa utengenezaji na baada ya utengenezaji • Kondomu zenye ubora maradufu na zilizofungwa sawa sawa hukaa ka takriban miaka mitano, au hata zaidi…