200 likes | 468 Views
KONDOMU. Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania. Ufanisi wa kondomu. Kitini hiki kimetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ , TBS na PSI-Tanzania. Utangulizi. Kuna watu wana wasiwasi kuhusu ufanisi wa kondomu.
E N D
KONDOMU Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na PSI-Tanzania.
Ufanisi wa kondomu Kitini hiki kimetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ , TBS na PSI-Tanzania
Utangulizi • Kuna watu wana wasiwasi kuhusu ufanisi wa kondomu. • Kuna ushahidi gani wa kisayansi unaoonyesha kuwa kondomu ni salama? • Hebu tuangalie tafiti mpya za kisayansi za hivi karibuni…
Kondomu inafanyaje kazi? • Kondomu huzuia • Uume kuguswa na majimaji toka kwenye uke;na uke kuguswa na majimaji kutoka kwenye uume; • hivyo, humlinda mwanaume na mwanamke
Kondomu inafanyaje kazi? • Kondomu zimetengenezwa • Kuvishwa kwa urahisi (kwenye uume) na • Kupunguza kuteleza na kupasuka wakati wa kujamiiana.
Mambo mawili inabidi yachunguzwe na wanasayansi; • 1) Je Kondomu, ikipimwa katika maabara, haipenyeshi vijdudu, hata virusi wadogo kabisa? • 2) Kuna ushahidi gani (tafiti) kuwa, matumizi ya kondomu hupunguza hatari ya kupata mimba, maambukizo ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa?
Swali la 1: Je, Kondomu hairuhusu vijidudu kupenya? • Hebu tuchambue tafiti za kisayansi zilizokwisha kuchapishwa • Je matundu yapo kwenye kondomu, zikichunguzwa kwa lensi kali? • Hapana,tafiti zote zilionyesha kutokuwapo kwa matundu.
Swali la 1: Je, Kondomu hairuhusu vijidudu kupenya? • Hata tafiti ya maabara kwa kutumia darubini kali inayokuza mara 30,000 haikupata vitundu. • Hata kondomu ikivutwa/tanuliwa, hakuna vitundu!
Swali la 1: Je, kondomu hairuhusu kupenya kwa vijidudu? • Je, tafiti kwa kutumia vijidudu pamoja na VVU zinasemaje? • Kondomu haina vitundu • Vipimo vya maabara ili kugundua kama vijidudu hupenya kwenye tabaka la kondomu, vilionyesha kutokuwa na uvujaji ama kupenya kwa vijidudu vya aina yoyote!!
Swali la 1: Kondomu hairuhusu kupenya kwa vijidudu? • Kuhitimisha, jibu la swali hilo ni ndio: Kondomu ya mpira ni kidhibiti bora dhidi ya kupenya kwa vijidudu vya maambukizo. • Kondom ni kinga thabiti dhidi ya kupenyeza wa virusi!!
Swali la 2: Matumizi ya kondomu hupunguza hatari ya maambukizo? • Tugeukie swali la pili: • Pamoja na kuwa vipimo vya maabara vinahakikisha kuwa kondomu ni bora, inabidi tuone kama matokeo haya yanathibitishwa na tafiti za kijamii. • Je,matumizi ya kondom yanathibitisha ufanisi wa kondomu
Kinga dhidi ya VVU/UKIMWI • Tafiti za wenzi- mmoja aliyeambukizwa VVU na mmoja ambaye hajaambukizwa zinaonyesha ni jinsi gani kondomu zilivyo fanisi: • Tafiti zote zinaonyesha kuwa, watumiaji wa kondomu wana hatari ndogo ya kuambukizwa VVU: • Tafiti mpya 3 ziligundua kuwa, maambukizi kati ya wenzi wenye VVU yalikuwa pungufu kwa 1% kwa mwaka kati ya wale waliotumia kondomu kila mara.
Kinga dhidi ya VVU/UKIMWI • Tafiti kubwa ya Ulaya, kati ya wenzi 256 wenye VVU, ilionyesha kuwa, katika kipindi cha miezi 20, hapakuwa na ambukizo hata moja kati ya wenzi waliotumia kondomu kila mara • Ukilinganisha na wenzi 12 kati ya 121 ambao hawakutumia kondomu kila mara, walipata maambukizo. • Hivyo basi, tafiti zinathibitisha kuwa, kondomu ni kinga bora dhidi ya VVU/UKIMWI!!
Kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa • Kondomu hukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa: • Tafiti ya hivi karibuni (2004) iliyofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ilithibitisha kuwa kondomu ni kinga thabiti kwa wanaume na wanawake dhidi ya maambukizo ya chlamydia, kaswende, kisonono na virusi vya herpes aina ya pili. • Tafiti zote zilichunguzwa kwa makini na tafiti zenye ubunifu kasoro kuachwa.
Ufanisi katika kuzuia mimba • Wanawake 3 hadi 14 kati ya 100 hupata mimba baada ya mwaka watumiapo kondomu kama kinga pekee • Hata hivyo, upungufu huu kwa kondomu hutokana na binadamu kushindwa kutumia kondomu kwa usahihi, na kila mara.
Ufanisi katika kuzuia mimba • Upungufu katika kuzuia mimba unaweza kusababishwa na; • Kutokupatikana kwa kondomu • Hawatumii Kondomu kila mara na ipasavyo • Aibu/kutokuwa wazi kati ya wenzi • Mtumiaji kutokujua namna ya kutumia kondomu kwa usahihi.
Ufanisi katika kuzuia mimba • Mfano, hatari ya kupasuka inatokea kwa wapenzi ambao hawana elimu ya matumizi ya kondomu.. • Asilimia kubwa ya wenzi watumiao kondomu kila mara wana hatari ndogo ya mimba.
Hitimisho la ufanisi wa kondomu • Kondomu ikitumika kila mara na ipasavyo/kwa usahihi hupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya ngono na VVU pamoja na kuzuia mimba zisizotarajiwa.
Hitimisho la ufanisi wa kondomu • Kushindwa kwa kondomu kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa pamoja na VVU hutokana na mtumiaji kushindwa kuitumia ipasavyo na wala sio ubora wake. • Hivyo inabidi uhamasishaji wa matumizi sahihi ufanyike kila mara.
Hitimisho la ufanisi wa kondomu • Imani potofu kuhusiana na kondomu zinapotosha hivyo inabidi ushahidi wa kisayansi uzingatiwe. • Matumizi ya kondom lazima yafundishwe na pia waweza kujifunza kwa kutuimia.