220 likes | 565 Views
NENO LA UZIMA April 2013. Ndugu, msinung’unikiane (Yak 5:9). Ili tulielewe vizuri zaidi Neno hilo la mwezi huu lazima tuangalie mazingira lilimokusudiwa. Ni matatizo yaliyoibuka katika jumuia za Kikristo waliopelekewa waraka wa Mtume Yakobo.
E N D
NENO LA UZIMA April 2013
Ili tulielewe vizuri zaidi Neno hilo la mwezi huu lazima tuangalie mazingira lilimokusudiwa. .
Ni matatizo yaliyoibuka katika jumuia za Kikristo waliopelekewa waraka wa Mtume Yakobo. .
Yalikuwa makwazo, ubaguzi wa kijamii, matumizi ya kibinafsi ya mali, kunyanyasa wafanyakazi, imani ambayo ilikuwa zaidi ya maneno kuliko matendo, n. k.
Hayo yote yalisababisha machukizo na malalamiko ya wao kwa wao, na hivyo kujenga hali ya mahangaiko kaika jumuia nzima. .
Tayari tangu nyakati za miume waliweza kutambua yale tunayoona katika jumuia zetu:
matatizo makubwa zaidi ya kuweza kuishi imani yetu, mara nyingi si matatizo yanayotokana toka nje, yaani toka dunia, bali ni yale yatokanayo toka ndani:
hali fulani zitokanazo na mwenendo mbalimbali wa ndugu zetu, usiolingana na kipeo cha Kikristo.
Lakini, ikiwa upinzani na udhia hizo zilizo mbaya kiasi au vikubwa, zina mizizi katika imani ambayo mara nyingine haimulikwi, na upendo hafifu sana kwa Mungu na kwa jirani, basi Mkristo anapaswa mara, kuacha kuuzika na kupinga vikali, bali vile anavyofundisha Yesu.
Yeye anataka tungoje kwa uvumilivu, kuwaelewa, na kuwa na huruma, ambazo zinasaidia kuchipusha mbegu ile ya wema uliopandwa ndani yetu, unavyofundisha mfano wa magugu (Mt 13:24-30. 36-43).
Tuishije, basi, Neno la Uzima la mwezi huu? Neno hilo linatuweka mbele ya hali ngumu ya maisha ya Kikristo. .
Ijapo tunashiriki na jumuia mbalimbali (kama familia, parokia, shirika, mazingira ya kazi, jumuia ya mwananchi), ambamo, kwa bahati mbaya, kuna mengi yasiyopendeza.
Kama tabia ya watu, maono tofauti, mwenendo wa watu, mambo kinyume yanayohuzunisha na kutusababisha upinzani.
Tazama, basi, nafasi mbalimbali nyingi za kuishi vema Neno hilo la Uzima la mwezi huu.
Mahali pa manung’uniko au kuhukumu – tunavyoelekezwa kufanya – tutaweka saburi na maelewano; halafu, kadiri inavyowezekana, hata maonyo ya kidugu;
na hasa tutatoa ushahidi wa Kikristo, kwa kuzidisha kwa uwingi wa upendo na kuwajibika, kwa upande wetu, mbele ya ukosefu wa upendo au kuwajibika unaoweza kutokea.
Ndugu, msinung’unikiane (Yak 5:9) “Parola di Vita” inatangazwa na MovementofFocolare. Matini hii Imetolewakatika Città Nuova, n.22/1989Chapa cha Anna Lollo akishirikiana na Fr. PlacidoD’Omina (Sicily, Italy). Maelezo ya Neno la Uzima inatafsiriwa katika lugha 96 na kilugha na kuwafikia mamilioni ya watu katika dunia nzima kwa njia ya maandishi, radio, TV na kwa njia ya Tovuti. Kwa kupata maelezo www.focolare.org PPS hiyo, katika lugha mbalimbali inatangazwa katika www.santuariosancalogero.it (na hapo unaweza kupakua)