190 likes | 420 Views
NENO LA UZIMA. Mei 2012. "Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!” (Lk 12:49). Katika maandishi ya kiyahudi moto unaashiria neno la Mungu lililotamkwa na nabii. Lakini pia linaashiria hukumu ya Mungu anayetakasa watu wake kwa kupita kati yao.
E N D
NENO LA UZIMA Mei 2012
"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!” (Lk 12:49).
Katika maandishi ya kiyahudi moto unaashiria neno la Mungu lililotamkwa na nabii. Lakini pia linaashiria hukumu ya Mungu anayetakasa watu wake kwa kupita kati yao..
Tunaweza kusema hivyo kwa neno la Yesu: linajenga, na kwa wakati huo huo linabomoa kila kisicho thabiti, kila kinachotakiwa kushuka, kila kilicho batili, na kuacha tu ukweli ukisimama.
Yohani Mbatizaji alisema: “Atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na moto” (Lk 3:16), akitabiri ubatizo wa Kikristo uliozinduliwa siku ya Pentekoste kwa kushuka Roho Mtakatifu na kuonekana ndimi za moto (rej Mdo 2:3).
Hii ni kazi maalum ya Yesu: kuwasha moto duniani, kuleta Roho Mtakatifu na nguvu zake za kufanya upya na kutakasa. Huo ndio utume wa Yesu: kutupa moto duniani, kuleta Roho Mtakatifu pamoja na nguvu yake ya kufanya yote upya na ya kutakasa.
"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!” (Lk 12:49).
Yesu anatupatia Roho. Lakini Roho Mtakatifu anafanyaje kazi?
Anatujaza upendo na anataka tutunze moto huu wa upendo ukiwaka mioyoni mwetu.
Je, ni aina gani ya upendo? Si wa kiulimwengu, upendo usio na kikomo. Ni upendo wa kiinjili. Unaopenda wote kama Baba wa mbinguni anayewaangazia jua lake waovu na wema na kuwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki, wakiwemo adui (rej Mt 5:45).
Ni upendo usiosubiri wengine wachukue hatua ya kwanza, bali unakuwa daima wa kwanza kupenda.
Ni upendo unaojifanya mmoja na kila mmoja: unateseka na kufurahi pamoja nao, ukishiriki hofu na matumaini yao. Na ikibidi, unagusika, kwa matendo. Kwa hiyo siyo tu upendo wa kihisia unaoelezwa kwa maneno matupu.
Ni upendo unaoongozwa na Kristo ndani ya jirani, kwa kuzingatia maneno yake: ‘Ulinitendea mimi” (Mt 25:40). Ni upendo unaopelekea upendano.
Kwa kuwa upendo huu unaonekana, ni udhihirisho wa maisha yetu ya kiinjili, unasisitiza na kushuhudia neno - ushuhuda tunaoweza na tunaotakiwa kutoa ili kuinjilisha.
"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!” (Lk 12:49).
Na moto lazima uunguze kitu daima. Na zaidi ya yote lazima uunguze ubinafsi wetu, na unafanikiwa kwa kuwa kwa kupenda tunaelekea nje yetu: aidha kuelekea Mungu kwa kufanya mapenzi yake, au jirani kwa kuwasaidia.
Hata moto mdogo, ukiwashwa unaweza kuwa mlipuko – ule mlipuko wa upendo, amani na undugu wa wote ambao Yesu alileta duniani.
"Nimekuja kuwasha moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi!” (Lk 12:49).