270 likes | 523 Views
Neno la Uzima. Mwezi Aprile 2012. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. (Yo 15, 3). Nadhani kuwa moyo wa mitume, waliposikia neno hilo la kutia moyo wa Yesu, uliruka kwa furaha. Jinsi ingekuwa heri, ikiwa Yesu anaweza kutwambia na sisi pia.
E N D
Neno la Uzima Mwezi Aprile 2012
Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. (Yo 15, 3)
Nadhani kuwa moyo wa mitume, waliposikia neno hilo la kutia moyo wa Yesu, uliruka kwa furaha.
Jinsi ingekuwa heri, ikiwa Yesu anaweza kutwambia na sisi pia. Ili tuweze kustahili kidogo, tujaribu kulielewa.
Yesu alikwisha kutumia mfano wa mzabibu na matawi. Yeye ni mzabibu wa kweli, Baba ni mkulima, anayeondoa kila matawi lisilozaa, na kusafisha kila tawi lizaalo, ili lizidi kuzaa.
Kisha kusema hayo, anaongeza: Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
Ni hali ile ya roho inayotakiwa ili kuweza kusimama mbele ya Mungu, isiyo na vizuio (kama kwa mfano dhambi) vinavyozuilia kukaribia matakatifu, kukutana na Mungu.
Hata katika Agano la Kale, mtu alitambua kwamba hawezi kumkaribia Mungu kwa nguvu zake tu. Alihitaji kuwa Mungu autakase moyo wake; kumpa moyo mpya.
Zaburi nzuri sana husema: “...Ee Mungu, uniumbie moyo safi”.
Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
Kwake Yesu kuna njia ya kuwa safi, nayo ni Neno lake. Neno lile ambalo wanafunzi walilosikia, na kulikubali, limewatakasa.
Naam, Neno la Yesu si kama maneno ya watu. Ndani yake yumo Kristo, jinsi, kwa namna nyingine, yumo katika Ekaristi. Kwa njia yake Kristo anaingia ndani yetu sisi. Tukilikubali na kutekeleza, linafanya kuwa Yesu azaliwe na kukua katika moyo wetu.
Baba Mtakatifu Paulo wa VI alikuwa akisema: “Anawezaje Yesu kuwemo katika roho za watu? Kwa njia ya kutushirikisha Neno, mawazo ya Mungu hupita, hupita Neno, Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu. Tungeweza kusema kuwa Bwana anachukua mwili ndani yetu tunapokubali kwamba Neno lije kuishi ndani yetu”.
Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
Neno la Yesu linafananishwa pia na mbegu iliyotupwa ndani ya mwumini. Lilipopokelewa, huingia ndani ya mtu na, kama mbegu, huchipuka na kukua, na kuzaa matunda, linatufanya “kuwa Kristo”, kwa kutufanya tufanane na Kristo.
Neno, likiingizwa na Roho Mtakatifu, lina kweli uwezo na nguvu ya kumshika Mkristo mbali na maovu: hadi anakubali kuacha Neno litende ndani yake, atakuwa huru na dhambi, basi atakuwa safi. Atatenda dhambi ikiwa anaacha kutii ukweli.
Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
Basi, tutaishije ili kustahili nasi sifa ya Yesu? Kwa kutekeleza kila Neno la Mungu, tukilishwa nalo saa hadi saa, kwa kufanya maisha yetu kuwa kazi ya uinjilishaji daima.
Hilo tupate kufika kuwa mawazo na hisia ya Yesu, kuishi yeye katika dunia, kumwonyesha katika jamii, ambayo mara nyingi imevurugwa na mabaya na dhambi, kuonyesha usafi wa kimungu, na mwangaza inaotupa Injili.
Halafu, katika mwezi huu, ikiwezekana (yaani ikiwa wengine wanashiriki nia zetu), tujitahidi kutekeleza kwa namna ya pekee lile neno linalodhihirisha amri ya mapendano
Mwinjili Yohane, anayeandika Neno la Yesu tulilotafakari leo, anaona ulingano kati ya Neno la Kristo na amri mpya. Kwake yeye, ni katika mapendano kwamba tunaishi Neno pamoja na matokeo yake ya usafi, utakatifu, tusitende dhambi, kuzaa matunda, kuwa karibu na Mungu.
Mtu katika upweke hawezi kudumu kushinda misukumo ya ulimwengu,
mbali katika mapendano hupatikana nafasi ya kufaa ya kulinda maisha ya Kikristo halisi.
Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. (Yo 15, 3) “Parola di Vita”, pubblicazione mensile del Movimento dei Focolari. Testo di: Chiara Lubich, scritta nel 1982 Grafica Anna Lollo in collaborazione con don Placido D’Omina (Sicilia, Italia) Questo commento alla Parola di Vita è tradotto in 96 lingue e idiomi, e raggiunge vari milioni di persone in tutto il mondotramite stampa, radio, TV e via internet.Per informazioni www.focolare.orgQuesto PPS, in diverse lingue, è pubblicato su www.santuariosancalogero.org (da dove si può scaricare)