390 likes | 701 Views
TAARIFA YA HALI YA KILIMO NA CHAKULA YA MKOA WA MWANZA MEI 2008. ILIYOWASILISHWA KATIKA KAMATI YA SIASA YA CCM YA MKOA MWEZI MEI 2008 Na: Mh. Dr. J.A. Msekela (Mb). 1. Utangulizi.
E N D
TAARIFA YA HALI YA KILIMO NA CHAKULA YA MKOA WA MWANZA MEI 2008 ILIYOWASILISHWA KATIKA KAMATI YA SIASA YA CCM YA MKOA MWEZI MEI 2008 Na: Mh. Dr. J.A. Msekela (Mb)
1. Utangulizi Mkoa wa Mwanza una eneo la kilomita za mraba 35,187 ambapo asilimia 43 ni eneo la maji. Eneo la nchi kavu ni kilomita za mraba 20095 sawa na hekta 2,009,500. Mkoa una wilaya nane ambazo ni Geita ,Sengerema, Misungwi, Kwimba, Magu, Ukerewe, Ilemela na Nyamagana.Vilevile mkoa una tarafa 33, kata 174 na vijiji 706. Mkoa unakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni 3.5 na mahitaji chakula yanayokadiriwa kufikia tani 868,500 za chakula aina ya wanga na tani 375000 za chakula aina ya protini.
2. Hali ya hewa -1. • Mkoa hupata mvua za aina mbili (Bimodal rainfall partern) kwa mwaka yaani mvua za vuli (Short rain) na mvua za masika (long rain). Mvua za vuli huanza mwezi Oktoba kwa wilaya za Geita ,Sengerema na Ukerewe na wilaya zilizobaki mvua huanza mwezi Novemba. Mvua hizi huendelea hadi mwezi Februari katikati na baada ya hapo panakuwepo na kiangazi kifupi(short dry spell). Mvua za masika huanza mwanzoni mwa mwezi Machi na huendelea hadi mwishoni mwa mwezi Mei. Kuanzia mwezi Juni hadi Agosti ni kiangazi.
3 Hali ya Hewa-2 • Takwimu za mvua zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka kumi, kuna miaka minne ya hali nzuri ya hewa, miaka mitatu ya hali mbaya ya hewa na miaka mitatu ya hali ya kawaida(wastani)
3. Eneo la kilimo. Mkoa wa Mwanza unalo eneo linalofaa kwa kilimo linalokadiriwa kuwa hekta 1,142,685 sawa na asilimia 32 ya eneo la mkoa na asilimia 57 ya eneo la nchi kavu. Eneo linalotumika kwa kilimo ni hekta 740,000 sawa na asilmia 64.7 ya eneo la kilimo.Wastani wa eneo la ardhi iliyopo kwa kaya ni hekta 3.5 na wastani wa eneo la kilimo kwa kaya ni hekta 2. Majedwali yafuatayo yanaonyesha hali halisi ya idadi ya watu , kaya na eneo la ardhi kwa matumizi ya kilimo
4. 4. Hali ya uzalishaji wa mazao ya kilimo • . • Uzalishaji wa mazao kilimo bado uko chini ikilinganishwa na uzalishaji ambao ungepatikana kama wakulima wangefuata kanuni za kilimo bora cha mazao walimayo.
5.0 Upatikanaji wa pembejeo za kilimo • Pembejeo za kilimo muhimu mkoani ni mbolea ,madawa na mbegu bora.Pembejeo hizi zinaendelea kupatikana kwa mawakala binafsi ambao huleta kufuatana na mahitaji na kasi ya ununuzi kutoka kwa wakulima. Hata hivyo pembejeo nyingi zinapatikana makao makuu ya mkoa ,chache makao makuu ya wilaya, na chache sana au hakuna kwa maeneo ya vijijini.
5.1 Pembejeo zenye ruzuku msimu 2007/08. • Msimu wa kilimo 2007/08, mkoa haukupewa mbolea ya ruzuku bali ulipewa mahindi aina ya Longe 4 yenye ruzuku na madawa ya pamba.
5.1.1 Mahindi yenye ruzuku. • Mkoa ulipangiwa tani 40 za mahindi yenye ruzuku.Kiasi cha tani 20.04 ndicho kilicholetwa mkoani hapo tarehe 06/02/2008.Hadi mwezi April 2008, kiasi cha tani 10 ndicho kilikuwakimeishanunuliwa na mawakala kutoka mawilayani.Mbegu hii hununuliwa Jijini Mwanza kwa Tsh 700 kwa kilo na huuzwa kwa wakulima wilayani kwa bei ya Tsh.800-900 kwa kilo kutegemeana na gharama za usafirishaji kutoka Jijini Mwanza hadi wilaya husika.
5.1.2 Madawa ya Pamba yenye ruzuku. • Serikali ilitoa fedha kwa Bodi ya Pamba kwa ajili ya ruzuku ya madawa ya pamba.Kutokana na ruzuku hiyo , bei ya madawa haya imeteremka kutoka Tsh3000 kwa acrepack moja msimu uliopita hadi Tsh.2100 msimu huu.
Jedwali na.5:Mahitaji, upatikanaji wa usambazaji wa pembejeo 2007/08
6.Kilimo cha umwagiliaji. • Kutokana na kuwepo kwa maji ya kutosha yanayotokana na ziwa Victoria, mito na maeneo tambarare, mkoa una eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji linalokadiriwa kufikia hekta 30,023.Pamoja na mkoa kuwa na eneo kubwa linalofaa kwa kilimo hiki , eneo lililoendelezwa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta 2464 sawa na asilimia 8.2
7. Matumizi ya zana kilimo. • Lengo la matumizi ya zana za kilimo ni kurahisisha na kuharakisha shughuli za kilimo kwa kutumia trekta, matrekta madogo ya mkono(power tiller) na jembe la kukokotwa na ngombe .Hadi sasa mkoa unakadiriwa kuwa na matrekta 190 na plau za kukokotwa na ngombe zipatazo 30,282. Inakadiriwa kuwa asilimia 2.8 ya wakulima mkoani hutumia trekta, asilimia 32.3 hutumia plau(jembe la kukokotwa na wanyama) na asilimia 64.9 hutumia jembe la mkono.
8. Huduma za ugani • Huduma za ugani zinafanywa na watumishi 484. Idadi hii ni ndogo ikilinganishwa na eneo la mkoa lenye kata 175 na vjiji 706. Vilevile watumishi wenye taaluma ya kilimo kati ya hao ni 207.
9.0 Hali ya kilimo na chakula msimu 2007/2008 • 9.1 Hali ya hewa. • Hali ya hewa msimu sio ya kuridhisha kwani mvua za vuli zilikuwa kidigo na mtawanyiko wake haukuwa mzuri(baadhi ya maeneo hayakupata mvua za kutosha).Mvua za masika nazo sio za kuridhisha kwani zinanyesha mara chache na kuambatana na vipindi virefu vya jua.Hata hivyo zinaonyesha dalili za kumalizika/kukatika mapema badala ya kunyesha hadi mwishoni mwa mwezi Mei 9.0
Hali ya kilimo na chakula msimu 2007/2008-inaendelea • Hali hii imeathiri ustawi wa mazao mashambani na hasa zao la mpunga ambalo huhitaji mvua nyingi.Msimu uliopita(2006/07)zao la mpuga lilipatikana kwa wingi kutokana na mvua nyingi.
Utekelezaji wa Malengo ya Kilimo: • Msimu 2007/2008 Mkoa ulilenga kulima hekta 603,470 za mazao ya chakula zenye kutarajia kutoa mavuno ya tani 995,652 na hekta 140,873 za zao la pamba zenye kutarajia kutoa mavuno ya tani 211,305. • Hadi mwezi Machi 2008, hekta 449,637 za mazao ya chakula zilikuwa zimelimwa. Hii ni sawa na asilimia 74 ya lengo. Eneo hili linakadiriwa kutoa mavuno ya tani 780,928 za chakula sawa na asilimia 78 ya lengo. Vile vile hekta 71,845 za zao la pamba zilikuwa zimelimwa, hii ni sawa na asilimia 51 ya lengo. Eneo hili linakadiriwa kutoa mavuno ya tani 89,809 za pamba mbegu.
Jedwali Na.9: Utekelezaji wa malengo ya kilimo hadi Machi, 2008:-
Hali ya chakula. • Hali ya chakula ni ya kuridhisha kwa maeneo mengi ya mkoa kwani chakula kinapatikana katika masoko na magulio kwani hiki ni kipindi cha mavuno, isipokuwa bei ndizo zipo juu. Bei kuwa juu inatokana na hali ya kutokuwa nzuri hivyo kufanya uzalishaji wa baadhi ya mazao kuwa chini.Mfano msimu uliopita mkoa ulizalisha mpunga kwa wingi(tani 268,205) ilamsimu huu(2007/08) kiasi cha tani 122,240 ndicho kinakadiriwa kuzalishwa. Mkoa huhitaji chakula kinachokadiriwa kufikia tani 865,000 za chakula aina wanga na tani 375,000 za chakula aina ya mikunde.Ili kuweza kujitosheleza kwa chakula uzalishaji wetu ni muhimu ufikie kiwango hicho.
Jedwali Na.11: Ulinganisho wa bei za vyakula kwa miaka miwili
10.Zao la biashara (pamba). • Msimu uliopita mkoa ulizalisha kilo 41,814,749 za pamba. Uzalishaji ulikuwa kidogo kutokana na mvua nyingi zilizonyesha msimu uliopita.Bei ya kununulia pamba ilikuwa Tsh.350-550 kwa kilo.Bei ya Tsh 550 haijawahi kupatikana tangu kilimo cha zao la pamba kianze mkoani. • Msimu huu (2007/08) tunategemea kuzalisha kilo 80,000,000. za pamba.
Jedwali na. 12: Uzalishaji wa pamba kwa kipindi cha misimu 6
11.Utekelezaji wa mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo(ASDP) • Mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo unatekelezwa kupitia programu ya kuendeleza kilimo (Agricultural Sector Development Programme-ASDP). Ngazi ya wilaya mkakati huu unatekelezwa kupitia mipango ya maendeleo ya kilimo wilayani (District Agricultural Development Plans –DADPs).
11.Utekelezaji wa mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo - unaendelea Mwaka 2006/07 miradi 66 ya sekta ya kilimo, mifugo na ushirika yenye thamani ya Tsh.1,005,257,923 ilitekelezwa. Baadhi ya miradi iliyotekelzwa ni kama ifuatavyo; • Ukarabati wa majosho • Uanzishwaji na uimarishaji wa SACCOS. • Ununuzi wa pampu za umwagilaji kwa ajili ya vikundi vya wakulima • Ukarabati wa machinjio • Kutoa mafunzo kwa wakulima na maafisa ugani • Ununuzi wa mbegu za mihogo zenye kustahimili ugonjwa wa mihogo • Ununuzi wa mbuzi wa kisasa ili kuboresha wa kienyeji
Jedwali na 13. Fedha zilizotolewa mwaka 2006/07 kwa kila wilaya ni kama ifuatvyo;
Aidha mwaka 2007/2008 miradi ya kilimo , ushirika na mifugo ipatayo 78 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.6 imepangwa kutekelezwa mkoani. • Baadhi ya miradi iliyopangwa kutekelezwa ni; • Ukarabati wa majosho • Ununuzi wa mbegu za mihogo zinazostahimili ugonjwa wa batobato kali • Ukarabati wa miradi ya umwagiliaji • Ukarabati wa malambo ya maji kwa ajili ya mifugo • Mafunzo kwa wakulima kuhusu kanuni za kilimo bora za mazao walimayo
Mafunzo kwa wanachama wa vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) • Ununuzi wa vitendea kazi • Uimarishaji wa kilimo cha bustani • Uimarishji wa ufugaji bora wa kuku • Ukarabati wa machinjio • Ujenzi wa masoko(market centres) • Ukarabati wa vituo vya maksai(oxenazation centres)
Mafunzo kwa wakulima kuhusu matumizi ya jembe la kukokotwa na wanyama • Ukarabati wa machinjio • Ununuzi wa pampu za umwagiliaji kwa ajili ya kuvipatia vikundi vya umwagiliaji • Ununuzi wa vitendea kazi mfano kompyuta, pikipiki, na baiskeli
Aidha yapo matatizo yanayokabili utekelezaji wa mpango huu kama ifuatavyo; • 1. Elimu ndogo ya wakulima katika kuibua miradi yenye manufaa • 2. Fedha huchelewa kufika mawilayani. • 3. Taratibu za zabuni huchukua muda mrefu hivyo kufanya shughuli zilizopangwa kutofanyika mapema. • 4. Miradi mingi midogomidogo huibuliwa hivyo kutokuwa na impact
12.Changamoto. • Ili kujitosheleza kwa chakula na kuinua kipato cha wananchi , mkoa unalenga kutatua changamoto zifuatazo: