310 likes | 527 Views
TAARIFA YA FEDHA YA MFUKO WA PPF KWA MWAKA WA FEDHA ULIOSHIA TAREHE 31 DISEMBA 2012. M.J. MMARI DIRECTOR OF FINANCE-PPF. AGENDA. UTANGULIZI MCHANGANUO WA TAARIFA ZA FEDHA ZA MFUKO WA PPF HADI KUFIKIA DISEMBA 2012 UTHAMINISHAJI WA MAFAO (ACTUARIAL VALUATION)
E N D
TAARIFA YA FEDHA YA MFUKO WA PPF KWA MWAKA WA FEDHA ULIOSHIA TAREHE 31 DISEMBA 2012 M.J. MMARI DIRECTOR OF FINANCE-PPF
AGENDA • UTANGULIZI • MCHANGANUO WA TAARIFA ZA FEDHA ZA MFUKO WA PPF HADI KUFIKIA DISEMBA 2012 • UTHAMINISHAJI WA MAFAO (ACTUARIAL VALUATION) • MFUMO WA MALIPO WA ELECTRONIC • CHANGAMOTO ZA UWASILISHAJI MICHANGO • HITIMISHO
UTANGULIZI • Mfuko wa PPF unaendesha mipango miwili ya pensheni ambayo ni mpango wa pensheni ambapo mafaou yanalipwa kwa kutumia fomula maalum (Traditional scheme) na mpango wa uwekezaji amana (Deposit Administration Scheme). Katika mipango yote miwili waajiri wanatakiwa kuwasilisha michango kwenye Mfuko .Mfuko huwekeza michango hiyo kwenye vitegauchumi mbalimbali ili kuweza kulipa mafao kwa wanachama.
UTANGULIZI..... • Mfuko una jukumu la kuwalipa wastaafu wa serekali malipo ya pensheni kwa niaba yake. • PPF imekuwa ikitoa taarifa za fedha kila mwaka na hesabu za mwisho zilizokaguliwa ni zile za mwaka unaoishia 31 Disemba 2012
UTANGULIZI..... • Taarifa hizi za fedha zilikaguliwa na kampuni ya Delloite and Touche kwa niaba ya Mkaguzi na Mdhibitu Mkuu (Controller and Auditor General). • Wakaguzi wa nje (CAG) walitoa hati safi kwa hesabu za fedha za mfuko kwa mwaka 2012.
UTANGULIZI….. • Taarifa za fedha ambazo zimekaguliwa zinajumuisha taarifa zifuatazo; • Taarifa ya Bodi ya Wadhamini • Taarifa ya Mabadiliko ya Rasilimali za Mfuko kwa mwaka 2012 (Statement of Changes in Net assets Available for Benefits)
UTANGULIZI….. • TaarifayaRasilimalizaMfukokwamwaka 2012 (Statement of Net assets Available for Benefits) • Taarifayamtiririkowafedhakwamwaka 2012 (Statement of Cash Flows) • Maelezoya kina juuyataarifazafedhayakijumuisha Sera zakihasibuzilizotumikakuandaamahesabupamojanaufafanuziwataarifazafedha.
UTANGULIZI….. • Pamoja na taarifa za fedha zilizoainishwa hapo juu taarifa ya mwaka ya Mfuko imejumuisha; • Taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini • Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu • Tamko la wajibu wa Bodi ya wadhamini juu ya uandaaji wa taarifa za fedha na • Taarifa ya wakaguzi wa nje.
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012 • Taarifa hii inatoa muhstasari wa mabadiliko Katika mwaka 2012 ikianzia na shughuli zinazohusu wanachama, mapato ya vitegauchumi na kumalizia na matumizi ya uendeshaji. • Shuguhuli zinazohusu wanachama ni pamoja na michango na mafao pia. Muhstasari wake ni kama unavyoonekana kwenye jedwali hapa chini;
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012….
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012… • Kwa upande wa michango mfuko wa PPF ulikusanya michango shilingi bilioni 229 mwaka 2012 ukilinganisha na shilingi bilioni 185 zilizokusanywa mwaka 2011, hii ni sawa na ongezeko la asilimia 24 Ongezeko la michango linatokana na ongezeko la wanachama wapya kwa mwaka 2012 na pia ongezeko la mishahara ya wanachama wa mfuko.
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012… • Kwa upande wa mafao mwaka 2012 mfuko ilipokea madai ya mafao yenye thamani ya shilingi 99.4 bilioni ukilinganisha na shilingi bilioni 71.9 mwaka 2011, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 38.
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012… • Mchanganuo wa mafao kwa mwaka 2011 ni kama ifuatavyo: • Asilimia 34 ( shilingi bilioni 33.5) ya mafao yalikuwa ni pensheni ya kila mwezi ambayo hulipwa kwa mwanachama aliyeondoka kazini kwa kutimiza umri wa kustaafu au aliyepunguzwa kazini pindi anapofikia miaka 55.
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012… • Aslimia 26 ( shilingi bilioni 25.7) ya mafao yalikuwa ni mkupuo wa pensheni, ambayo hulipwa mwanachama aliyestaafu kazi kwa umri au kupunguzwa kazi hata kama hajafikia umri wa miaka 55 ili mradi amechangia kwa muda usiopungua miaka 10. • Asilimia 19 ( shilingi bilioni 19.3) ya mafao ni mafao ya uwekezaji amana ambayo hulipwa kwa mwanachama aliyejiunga na mpango wa uwekezaji amana ili mradi ameondoka kwenye ajira.
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012… • Aslimia 16.5 ( shilingi bilioni 16.5) ya mafao yalikuwa ni mafao ya kujitoa, ambayo hulipwa mwanachama aliyeondoka kazini kwa kuacha au kuachishwa na mwajiri wake. • Asilimia 3.5 ( shilingi bilioni 3.5) ya mafao yalikuwa ni mafao ya kifo , ambayo hulipwa mwanachama aliyefariki akiwa kazini. • Mafao ya elimu yalikuwa asilimia 1.
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012… • Mapato yatokanayo na uwekezaji kwa mwaka 2012 baada ya kutoa gharama za uendeshaji na kodi ya mapato yalikuwa ni shilingi bilioni 93.2 ukilinganisha na shilingi bilioni 85.2 mwaka 2011 ambalo ni sawa ongezeko la asilimia 9.4.
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012…(Mchanganuowamapatoyatokanayonavitegauchumi )
TAARIFA YA MABADILIKO YA RASILIMALI ZA MFUKO KWA MWAKA 2012… • Mapatomengineyoyakijumuishaadayauwakalawakulipapenshenikwawastaafuwaserekaliyalikuwanishilingimilioni 2,509 ukilinganishanashilingimilioni 2,497 kwamwaka 2011 nisawanaongezeko la aslilimia 0.5. • Matumizi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za mfuko yalikuwa shilingi milioni 35,075 kwamwaka 2012, ukilinganishanashilingimilioni 31,128 kwamwaka 2011 nisawanaongezeko la asilimia 13. • Matokeo ya mabadiliko ya rasilimali kwa mwaka 2012 ni ongezeko la shilingi millioni 196,989 ukilinganisha na ongezeko la shilingi milioni 172,049 mwaka 2011.
TAARIFA YA RASILIMALI ZA MFUKO 31.DISEMBA 2012 • Madhumuni ya mifuko wa pensheni ni kujenga uwezo wa kifedha ili kuweza kulipa mafao ya wanachama wake watakapo fikia wakati wa kulipwa mafao. • Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2012 rasilimali za mfuko zilifikia shilingi milioni 1,091,515 kutoka shilingi milioni 894,526 mwaka 2011, hii ni sawa na ukuaji wa shilingi milioni 196,989 au asilimia 22.
TAARIFA YA RASILIMALI ZA MFUKO 31.DISEMBA 2012… • Mwaka 2012 rasilimali za mfuko zilizoelekezwa kwenye vitegauchumi ziliongezeka na kufikia shilingi milioni 1,023,125 (sawa na asilimia 93.7 ya rasilimali zote) ukilinganisha na shilingi milioni 837,664 (sawa na asilimia 93 ya rasilimali zote) mwaka 2011, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 22 kwa mchanganuo angalia jedwali lifuatalo
TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2012 • Taarifa hii inaonesha fedha taslimu zilizopokelewa na zile zilizolipwa kwa mwaka 2012. • Tofauti na taarifa hii taarifa ya Mabadiliko ya Rasilimali za Mfuko huonesha mapato na matumizi halisi hata kama mapato hayo hayajapokelewa au matumizi hayo hayajalipwa kwa mwaka 2012. • Taarifa hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza inaonesha mitiririko wa fedha kwenye shughuli za kawaida za mfuko, sehemu ya pili inaonesha mtiririko wa fedha kwenye shughuli za vitegauchumi na sehemu ya tatu ni kiasi cha fedha kilichokuwepo mwanzo na mwisho wa mwaka.
UTHAMINISHAJI WA MAFAO (ACTUARIAL VALUATION) • Mafao ya wanachama wa Mfuko wa PPF yanalipwa kwa kuzingatia kanuni za ukokotoaji zilizoainishwa kwenye sheria. • Kanuni za ukokotoaji mafao zinazingatia mshara wa mwisho ( wastani wa mishara ya mikubwa ya miaka mitano); muda wa mwanachama wa kuchangia kwenye mfuko na facta ya pensheni ambayo ni 1/600 ( ambayo inamaanisha kuwa kila mwaka mwanachama anahaki ya pensheni sawa na aslilimia 2 ya mshahara wake wa mwisho.
UTHAMINISHAJI WA MAFAO (ACTUARIAL VALUATION)... • Thamani ya mafao yaliyoahidiwa kwa wanachama wailo kwenye ajira na wale waliostaafu huwa haioneshwi kwenye mahesabu ya mfuko (kwenye taarifa ya rasilimali za mfuko), kwa mujibu wa taratibu za kihasibu.
UTHAMINISHAJI WA MAFAO (ACTUARIAL VALUATION)... • Ili kuondokana na adhari za mfuko kutokuwa endelevu, na kwa kuzingatia kuwa mwanachama anachangia kwa muda wote alioko kwenye ajira na atakuja kulipwa mafao baada ya kustaafu, ni lazima mafao yaliyoahidiwa kwa wanachama yafanyiwe uthamini. Hii inasaidia kubaini kama mfuko una uwezo wa kulipa mafao ambayo yameainishwa kwenye sheria kwa mujibu wa kanuni zilizoelekezwa.
UTHAMINISHAJI WA MAFAO (ACTUARIAL VALUATION)... • Uthamini wa mafao ya mfuko wa PPF hufanywa kila baada ya miaka mitatu, mara ya mwisho uthamini ulifanywa Disemba 2008. hata hiyo mfuko haukuweza kufanya tathmini ya mafao kwa mwaka 2012 kutokana na mthibiti kuwa na mchakato wa kuandaa kanuni za ukokotoaji wa mafao.
MFUMO WA MALIPO KWA KUTUMIA MTANDAO (ELECTRONIC PAYMENT) • Kuanzia mwezi wa sita mwaka jana malipo ya mafao ya wanachama yanalipwa moja kwa moja kwenye akaunti za wanachama kupitia mfumo wa citi direct. • Mfumo huu umepunguza matumizi ya hundi na kuongeza ufanisi katika ulipaji wa mafao, haswa pale anayelipwa ana akaunti na benki ambayo sio zile ambazo mfuko una akaunti nazo.
CHANGAMOTO ZA UWASILISHAJI MICHANGO • Uwasilishaji michango ya wanachama umekuwa na changamoto kuu mbili; • Moja ni kuchelewa kuwasilisha michango • Pili ni michango kuwasilishwa mojakwa moja kwenye akaunti za benki za PPF bila kuleta majedwali ya michango pamoja na uthibitisho wa kufanya malipo kwenye akaunti za benki za PPF.
CHANGAMOTO ZA UWASILISHAJI MICHANGO ... • Tunatoa rai kwa wanachamna wetu kuwasilisha michango kwa wakati na kuleta majedwali ya michango (kwa mtandao) pamoja deposit slip/transfer confirmation ili tuweze kuwapatia stakabadhi ya malipo. Pia kwa urahisi wanachama wanashauriwa kutumia tuvuti ya mfuko kuwasilisha taarifa za michango.
HITIMISHO • Mfuko wa PPF umeendelea kuwa na ufanisi mkubwa na pia matokeo mazuri ya kifedha na kiutendaji mwaka hadi mwaka. • Taarifa za fedha za mwaka 2012 zimepata hati safi ya wakaguzi. • Uthamini wa mafao umeonyesha kuwa uwezo wa mfuko wa kutoa mafao kwa wanachama kwa mujibu wa kanuni za PPF ni endelevu.