270 likes | 478 Views
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA. Mkutano wa Mwaka wa Majadiliano ya Sera za Kupunguza Umaskini na Matumizi ya Rasilimali za Umma, 19 – 21 Novemba, 2008, Dar Es Salaam. DONDOO. Usuli Utangulizi Mafanikio Changamoto Masuala ya Mjadala. 1.0. USULI.
E N D
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MKUKUTA Mkutano wa Mwaka wa Majadiliano ya Sera za Kupunguza Umaskini na Matumizi ya Rasilimali za Umma, 19 – 21 Novemba, 2008, Dar Es Salaam.
DONDOO • Usuli • Utangulizi • Mafanikio • Changamoto • Masuala ya Mjadala
1.0. USULI • MKUKUTA unatekelezwa kupitia michakato ya serikali, Programme za mageuzi/maboresho na programu za maendeleo za kisekta • Hatua zinazochukuliwa na asasi zisizo za kiserikali (Sekta binafsi, mashirika ya hiari, vyama vya wafanyakazi, taasisi za kidini) • Hivyo, Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA imeandaliwa kutokana na taarifa za utekelezaji za wadau hawa.
2.0. UTANGULIZI • Taarifa ya Utekelezaji wa MKUKUTA (2007/8) inatoa sura ya jumla ya mafanikio, changamoto, mambo tuliyojifunza na hatua zinazofuata katika kutekeleza nguzo zote tatu za MKUKUTA • Hatua zilizofikiwa katika • Ugharimiaji, ufuatiliaji na tathmini • Michakato na mageuzi na jinsi hatua hizi zilivyochangia kufikiwa kwa matokeo ya MKUKUTA • Taarifa hii imezingatia uwepo wa Taarifa za Utekelezaji za MDAs na za wadau wasio wa kiserikali
…Inaendelea • Taarifa hizi zinatoa hatua zilizochukuliwa na mafanikio kwa kina zaidi • Kwa maeneo fulani takwimu hazijabadilika sana ikilinganishwa na taarifa ya 2006/7 • Aidha katika baadhi ya maeneo takwimu za karibuni hazikupatikana hasa zile zinazotokana na savei. • Taarifa hii imejikita zaidi katika kipindi cha hadi Juni 2008 • Lengo kuu la Ripoti hii ni kutoa taarifa ya hatua zilizofikiwa na kuamsha majadiliano kwa ajili ya kuboresha hatua zinazofuata.
3.0. MAFANIKIO: Ukuaji wa Uchumi na Kupunguza Umaskini wa Kipato • Serikali imeendelea kutekeleza sera, mikakati na mageuzi kwa lengo la kuimarisha uchumi • Viashiria vingi vinaonyesha mwelekeo mzuri • Mfumuko wa bei umepungua kutoka asilimia 7.3 (2006) hadi 7.0 (2007) ingawa ni juu ya lengo la MKUKUTA la asilimia 5 • Makusanyo ya kodi kama asilimia ya pato la taifa yameongezeka • Mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka katika mwaka 2007/8 • Deni la taifa limeongezeka lakini endelevu • Thamani ya uwekezaji kutoka nje imeongezeka • Ajira mpya 437,205 zimepatikana • Pato la taifa limeongezeka na hivyo pato la wastani la mwananchi
2.2. Ubora wa Maisha na Ustawi wa Jamii • Hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ili kuboresha maisha na ustawi wa jamii • Elimu – utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu umeendelea kutoa mafanikio mazuri • Elimu ya Awali • Idadi ya watoto walioandikishwa (Net) imeongezeka kutoka asilimia 33.1 hadi 36.2 Gross kutoka asilimia35.2 hadi38.1 mwaka 2008 • Idadi ya watoto wenye ulemavu walioandikishwa imeongezeka kutoka 685 hadi 2146
…Inaendelea • Elimu ya Msingi • Watoto walioandikishwa darasa la kwanza (Net) imefikia asilimia 97.2 • Wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari imefikia asilimia 56.7 • Watoto yatima walioandikishwa wameongezeka kutoka 748,641 (2007) hadi 915,234 (2008) • Watoto wenye ulemavu walioandikishwa wameongezeka kutoka 24,003 (2007) hadi 34,661(2008)
…Inaendelea • Elimu ya Sekondari • Wanafunzi wanaoingia sekondari (NER) imefikia asilimia 23.5. Lengo la MKUKUTA ni asilimia 25 kufikia mwaka 2010 • Elimu ya Juu • Idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu wamefikia 75,346 (wasichana ni asilimia 35)
…Inaendelea • Afya • Programu mbalimbali zimeendelea kutekelezwa katika sekta ya Afya chini ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) • Elimu ya kinga • Kampeni za chanjo • Kuzuia maambukizo • Pamekuwa na mafanikio kadha katika eneo la afya ya mtoto na mama • Watoto waliochanjwa wakati wa kuzaliwa wamefikia asilimia 73 • Wagonjwa wa malaria wameendelea kupungua na hivyo kupelekea kupungua kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano • Hata hivyo kumekuwa na tofauti ya matokeo haya kati ya mijini na vijijini • Chanjo ya surua imefikia asilimia 85 • Vifo vya kinamama bado viko juu (hakuna takwimu mpya)
…Inaendelea • VVU/UKIMWI • Juhudi zimeendelea kufanyika kupambana na UKIMWI chini ya Tume ya UKIMWI na Programu ya kudhibiti UKIMWI (NACP) • Usimamizi wa mambukizo yanayotokana na zinaa • Kupima na ushauri nasaha wa UKIMWI • Kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto • Asilimia 47 ya mama wajawazito walipata huduma ya kupima UKIMWI kwenye vituo vya PMTCT kufikia Desemba 2007 • Asilimia 34 ya wliopatikana na VVU walipatiwa dawa ya ARV kuzuia maambukizi kwa mtoto
…Inaendelea • Sekta ya Maji • Serikali imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji • Maji vijijini • Maji mijini • Maji taka • Kumekuwepo na ongezeko dogo ya idadi ya watu wanaopata maji safi na salama vijijini • Takwimu za savei zinaonyesha kuwa pamekuwa na kupungua kwa asilimia ya wanaopata maji safi na salama • Hali ni mbaya zaidi kwa upande wa jiji la Dar Es Salaam
…Inaendelea • Kinga ya Jamii • Serikali inakamilisha mwongozo wa kinga ya jamii kwa ajili ya kuyashughulikia makundi yaliyo katika hatari ya kuathirika zaidi na umaskini • Katika mwaka 2007/8 serikali imeendelea kusaidia makundi yenye mahitaji maalum • Serikali imeendelea kuhudumia makazi 17 ya wazee • Imeendelea kuhudumia vyuo vitatu vya mafunzo (Vocational training colleges) kwa ajili ya watu wenye ulemavu • Serikali imesaidia mafunzo ya stadi watoto yatima 270 walio katika vituo vya kuwalelea (Remands and rehabilitation centres)
2.3. Governance and Accountability • Serikali imeendelea kutekeleza Mwongozo wa Utawala Bora • Maeneo muhimu ya mwongozo ni pamoja na • Ushiriki wa wananchi katika maamuzi yahusuyo maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi • Sekta binafsi na mwongozo wa udhibiti • Katiba, utawala wa sheria, usimamizi wa haki na kinga ya haki za binadamu
…Inaendelea • Usawa wa jinsia • Uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika usimamizi wa masuala umma • Demokrasia ya uchaguzi na • Utumishi wa umma
…Inaendelea • Hatua za kuridhisha zimefikiwa katika utekelezaji wa mwongozo • Serikali imepitia sheria 12 katika kipindi cha 2007/08 • Miswada 34 iliandaliwa ambapo miswada 23 ilipitishwa kuwa sheria • Serikali pia ilianzisha tovuti kwa ajili ya kupokea maoni/malalamiko ya wananchi
…Inaendelea • Serikali imeendelea kutekeleza utaratibu wa kupeleka madaraka zaidi kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (D by D) ili kuwa na utoaji bora wa huduma kwa umma • Wizara 14 zilitathminiwa ili kuona jinsi zinavyotekeleza na kuboresha utaratibu huu • Mchakato huu umeboresha matumizi ya fedha zilizopokelewa na LGAs • Mchakato pia umeongeza uwazi katika kutenga fedha na usahihi wa fedha zilizotegwa kwa shughuli mbalimbali
…Inaendelea • Vita dhidi ya rushwa iliendelea katika mwaka 2007/8 • Tuhuma 2,887 zilichunguzwa ambapo uchunguzi wa tuhuma 1009 ulikamilika • Kesi … zimefikishwa mahakamani katika mwaka 2007/8 • Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuboresha utumishi wa umma • Mapitio ya sera ya malipo ya muda wa kati • Kuajiri watumishi wapya 36,331 kutoka vyuo vikuu
…Inaendelea • Hatua pia zimeendelea kuchukuliwa kuimarisha uwezo mahakama • Kuongeza bajeti ya sekta • Ongezeko la Majaji wa Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa • Juhudi za kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa zimeendelea kuimarishwa • Kuongezwa kwa uwezo wa mabweni ya wafungwa magerezani • Kuboresha usafiri wa watuhumiwa wakati wa kesi zao
2.4. Ugharimiaji wa MKUKUTA • MKUKUTA unatekelezwa na wadau wote, hivyo na ugharimiaji wake • Serikali imekuwa ikitekeleza MKUKUTA kupitia bajeti yake kila mwaka • Mwongozo wa Mipango na Bajeti umeendelea kuhimiza utengwaji wa fedha kwa kuzingatia vipaumbele vya MKUKUTA • Katika mwaka 2007/8 asilimia 62.7 ya bajeti ilielekezwa kwenye vipaumbele vya MKUKUTA • Asilimia 49.37 (Nguzo ya I) • Asilimia 29.48 (Nguzo ya II) • Asilimia 21.15 (Nguzo ya II)
2.5. UFUATILIAJI NA TATHMINI • Shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya MKUKUTA imeendelea kutekelezwa kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji wa MKUKUTA, Mifumo ya Ufuatiliaji wa MDAs na ule Mamlaka za Serikali za Mitaa • Mfumo wa kitaasisi wa Ufuatiliaji (Kamati na Vikundi kazi) vimeendelea kutekeleza mipango yao ya kazi za ufuatiliaji wa MKUKUTA
…Inaendelea • Katika mwaka 2007/8 Mfumo umetoa taarifa mbalimbali • Ripoti ya Umaskini na Maendeleo ya Watu – 2007 • Ripoti ya Tathmini ya Utoaji Huduma Nchini • Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA • Kijarida cha MKUKUTA (Electronic) • Ushauri wa kisera • Aidha tafiti na savei mbalimbali zilifanyika • Mapato na Matumizi ya Kaya 2007
3.0. CHANGAMOTO • Changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa nguzo ya I • Kupanda kwa bei za petroli • Kutokuwa na nishati ya umeme yenye uhakika • Uwezo mdogo wa kutumia fedha za matengenezo ya barabara • Masuala ya manunuzi katika eneo la barabara (Procurement capacity, timing, planning etc) • Kutokuwa na utaratibu wa mikopo ya muda mrefu katika kilimo
…Inaendelea • Changamoto katika utekelezaji wa ubora wa maisha na ustawi wa jamii zinahusiana na • Masuala ya ubora wa huduma • Upatikanaji na gharama za huduma • Masuala ya rasilimali watu (Waalimu na Wauguzi) • Ongezeko la watu hasa makundi maalum (watoto yatima, watu wenye ulemavu, wazee) • Masuala ya manunuzi • Rasilimali fedha
…Inaendelea • Baadhi ya changamoto katika utawala bora na uwajibikaji ni pamoja na • Usimamizi na uratibu wa mageuzi hasa katika kupeleka majukumu kwenye Halmashauri na kupeleka wataalam • Kujenga uwezo wa halmashauri kumudu majukumu yanayohamishiwa • Utaratibu wa manunuzi unakwamisha
4.0. MASUALA YA MJADALA • Haya ni baadhi ya masuala yanayohitaji kupata maelezo sahihi ili kuchukua hatua zitakazosaidia kurebisha au kuongeza kasi • Lengo ni kuwezesha kuanzisha mijadala katika michakato ya kisera na mipango iliyopo ili kuboresha hatua zinazochukuliwa • Baadhi ya masuala ni pamoja na • Ukuaji endelevu wa uchumi na kupungua kwa umaskini • Kilimo cha kisasa na kupunguza umaskini
…Inaendelea • Nishati • Nishati mbadala • Nishati ya mimea na uhakika wa chakula • Elimu na Mkakati wa Kukuza Uchumi • Masuala ya idadi ya watu