270 likes | 433 Views
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara 2007. Baadhi ya matokeo ya Utafiti Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Yaliyomo. Utangulizi na Madhumuni ya Utafiti Viashiria vya sekta ya Jamii Nyumba, huduma za nyumbani na rasilimali za kaya Shughuli za uzalishaji na za kibenki
E N D
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara 2007 Baadhi ya matokeo ya Utafiti Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Yaliyomo • Utangulizi na Madhumuni ya Utafiti • Viashiria vya sekta ya Jamii • Nyumba, huduma za nyumbani na rasilimali za kaya • Shughuli za uzalishaji na za kibenki • Umaskini • Hitimisho
Sampuli • Sampuli ya Utafiti ilitokana na maeneo ya kuhesabia watu yalioyotumika katika Sensa ya Watu na Makazi 2002 • Kaya ziligawanywa katika matabaka ya kipato katika kila eneo ili kupata uwakilishi wa matabaka yote katika sampuli • Kaya zilizoingia katika uchambuzi ni 10,466 kati ya 10,752 zilizokusudiwa (97%) • Asilimia 12% ya kaya hizi ni kaya za akiba
Watu • Wastani wa idadi ya watu katika kaya umeonesha kupungua 4.9 hadi 4.8 • Idadi ya Kaya zinazoongozwa na wanawake imeongezeka • Kuna ongezeko la idadi ya watu wa umri wa miaka 65 na zaidi pia ambao wanaongoza kaya
Afya • Ikilinganishwa na Utafiti wa mwaka 2000/01: • Hakuna mabadiliko katika idadi ya wanakaya walioripoti kuugua au kujeruhiwa katika majuma 4 kabla ya utafiti; na hali hii ni kwa wote mjini na vijijini • Hakuna mabadiliko katika idadi ya waliotafuta huduma ya afya, ingawa • Kuna ongezeko katika waliotafuta huduma kutoka katika vituo vinavyomilikiwa na Serikali (55% hadi 65%) • Idadi ya walioripoti kuridhishwa na huduma katika vituo vya serikali imeongezeka ingawa ukosefu wa dawa uliripotiwa na wachache
Elimu • Ikilinganishwa na Utafiti wa mwaka 2000/01: • Kuna ongezeko katika idadi ya watu wazima wanaojua kusoma na kuandika • Kuna ongezeko kubwa la idadi ya watoto wa umri wa kwenda shule ambao wanakwenda shule za msingi na sekondari • Ongezeko katika idadi ya watoto walio katika darasa sahihi kulinganisha na umri
Nyumba na huduma za kaya • Ongezeko katika matumizi ya vifaa vya kisasa vya ujenzi • Hakuna mabadiliko katika idadi ya kaya zisizo na vyoo 7% • Upatikanaji wa maji safi na salama (hasa ya bomba) umeshuka
Uzalishaji katika kaya • Shughuli kuu za wanakaya: - kilimo kinaonesha kushuka - kuongezeka waajiriwa na waliojiajiri
Shughuli za kibenki katika kaya • Kumekuwa na ongezeko tangu mwaka 2000/01, la kaya ambazo zina wanakaya ambapo angalau: - mmoja na amiliki akaunti katika benki (ingawa idadi ilikuwa kubwa mwaka 91-02) - mmoja aliyechukua mkopo benki , - mmoja nayeshiriki katika vikundi vya kuweka na/au kukopa visivyo rasmi • Kwa ujumla idadi ya kaya za namna hii bado ni chache na zimejikita zaidi maeneo ya mjini
Hitimisho - I • Kuna maendeleo makubwa katika upande wa elimu, upande wa afya hakujawa na mabaidiliko makubwa katika matumizi ya huduma za tiba isipokuwa tu ongezeko katika utafutaji huduma katika vituo vya serikali • Kuendelea kudorora kwa huduma ya maji hasa maji ya bomba • Kuongezeka kwa ujenzi wa nyumba za kisasa na ongezeko la rasilimali katika kaya
Hitimisho - II • Kuendelea kupungua kwa wananchi wanaoshiriki katika kilimo na kuingia katika sekta nyingine • Tofauti ya kipato baina ya walionacho na wasionacho haijabadilika ambapo tofauti ni ndogo kwa watanzania waishio vijijini ikilinganishwa na wale wanaoishi mjini.
Mwisho Ahsanteni sana kwa kunisikiliza!