230 likes | 526 Views
Mikakati ya Kuvutia Uwekezaji ili kuimarisha na Kuendeleza uchumi Nchini. Yaliyomo. Muundo wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Kazi za Kituo cha Uwekezaji Huduma Zinazotolewa na TIC Muda wa Kupata Vibali vya uwekezaji Upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya Uwekezaji Vigezo Vikuu ili kusajili mradi
E N D
MikakatiyaKuvutiaUwekezajiilikuimarishanaKuendelezauchumiNchiniMikakatiyaKuvutiaUwekezajiilikuimarishanaKuendelezauchumiNchini
Yaliyomo • Muundo wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) • Kazi za Kituo cha Uwekezaji • Huduma Zinazotolewa na TIC • Muda wa Kupata Vibali vya uwekezaji • Upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya Uwekezaji • Vigezo Vikuu ili kusajili mradi • Vivutio vya Uwekezaji • Sababu za kuwekeza Tanzania • Mwenendo wa Usajili wa miradi • Fursa za Uwekezaji • Mikakati ya Kuvutia Uwekezaji • Changamoto • Mwisho
MuundowaKituo cha Uwekezaji (TIC) Serikali iliunda Kituo cha Uwekezaji chini ya sheria ya Uwekezaji (TIA, 1997) • Taasisi ipo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu na inasimimamiwa na Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji na Uwezeshaji • TIC inaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji chini ya mwenyekiti na wakurugenzi watano wa bodi ya utendaji • Makao makuu ya TIC yapo Dar es Salaam • TIC ina ofisi za kanda tatu: Moshi, Mbeya na Mwanza
Kazi za Kituo cha Uwekezaji Kituo cha Uwekezaji Kina majukumu yafuatayo:- • Kuhamasisha uwekezaji ndani na nje ya nchi • Kusaidia wawekezaji upatikanaji wa vibali na leseni mbali mbali zinazotolewa na taasisi za serikali kwa ajili ya miradi yao • Kuishauri Serikali kuhusu maswala mbalimbali yahusuyo Uwekezaji
Huduma zinazotolewa na TIC Mahala Pamoja (One Stop Shop) Taasisi zilizo Mahala pamoja (one stop shop) kwa ajili ya kusaidia wawekezaji kupata vibali mbalimbali ni:- • Usajili wa makampuni- (BRELA) • Utoaji wa leseni-(Viwanda na Biashara) • Idara ya uhamiaji • Wizara ya Kazi – vibali vya kufanya kazi nchini • Upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji- (Ardhi) • Huduma za kodi - TRA
Muda wa Kupata Vibali vya Uwekezaji Kibali Muda • Usajili wa Kampuni siku 3 • Leseni ya Kiwanda siku 1 • Leseni ya Biashara siku 1 • Cheti cha uwekezaji siku 7 • Hati ya Ukaazi daraja ‘A’ siku14 • Hati ya Ukaazi daraja‘B’ siku14 • Pass maalum siku 1
Upatikanaji wa Ardhi kwa Ajili ya Wawekezaji • Mwekezaji wa nje anapata hati ya kumiliki ardhi kutoka TIC yaani (Derivative Right) na mwekezaji wa ndani anapata hati ya kumiliki ardhi kutoka kwa Kamishna wa Ardhi. • Njia kuu mbili ambazo mwekezaji anaweza kupata ardhi A) Kuomba ardhi ya kijiji, kisha kufuata utaratibu wote unaotakiwa na hatimaye ardhi kuhaulishwa kutoka ardhi ya kijiji na kuwa ardhi ya Jumla ambayo itatayarishiwa hati na kupewa TIC, nayo TIC itaandaa Derivative Right kwa ajili ya mwekezaji.
Upatikanaji wa Ardhi kwa Ajili ya Wawekezaji B) Kununua ardhi kutoka kwa watu/Mashirika yanayomiliki ardhi. • Kutokana na utaratibu huu, baada ya makubaliano ya muuzaji na mnunuzi, muuzaji analazimika kurudisha Hati kwa Kamishna wa Ardhi ili Hati hiyo ifutwe na Hati mpya iandaliwe kwa jina la TIC. Baada ya hapo TIC inaandaa ‘‘Derivative Right’’ na kupewa mwekezaji. Mwekezaji wa ndani hahitaji Derivative Right, yeye anapata hati kutoka kwa kamishina wa Ardhi moja kwa moja
Vigezo vikuu vya kupatiwa cheti cha uwekezaji Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ambayo mwekezaji anapaswa atekeleze ili kupatiwa cheti cha Uwekezaji:- • Awe na kampuni iliyosajiliwa BRELA • Kuwasilisha mchanganuo wa mradi (Business Plan/Feasibility Study) unaoonyesha mradi una thamani isiyopungua dola za Kimarekani laki moja (USD 100,000); Kama mradi ni wa kampuni ya Mtanzania au Watanzania unapaswa • Kuwasilisha mchanganuo wa mradi (Business Plan/Feasibility Study) unaoonyesha mradi una thamani isiyopungua dola za Kimarekani laki tatu (USD 300,000) endapo kampuni inamilikiwa na wageni
VivutiovyaUwekezaji (TIA, 1997) • VivutiovyaKodi • BidhaazaMtaji i) UshuruwaForodha – 0% ii) VAT – 0% • MfanoMashine, matrektanaMitambo • BidhaazaMtaji (Deemed capital goods) i) UshuruwaForodha- Unasamehewa 75% ii) VAT – Unasamehewakwa 45% • Mfano: Majenereta, magari, majokofu, n.k
VivutiovyaUwekezaji (TIA, 1997) B) Vivutio visivyo vya Kodi • Ruhusa ya kuajiri wafanyakazi wageni hadi watano endapo watahitajika. • Ruhusa ya kusafirisha faida baada ya kulipa kodi zote
Sababuzakuwekeza Tanzania BaadhiyaSababuzinazofanyawawekezajiwaamuekuwekezaNchini: • Amaninautulivuwa Tanzania • Mahaliilipo Tanzania; Kijiografianirahisikusafirishabidhaambalimbalinjeyanchikupitiabandarizetuza Dar es salaam, TanganaMtwara. Pianirahisikuuzabidhaakwendanchiambazohazijapakananabahari. • VivutiovizurivyaUwekezaji • Tanzania nimwanachamawachombokinachoitwa MIGA ambachohuwaakikishiawawekezajiusalamawamalizaodhidiyautaifishaji.
Sababuzakuwekeza Tanzania • EndapokunatokeamigogorokatiyamwekezajinaSerikalinamuafakakutofikiwa, mwekezajianawezakupelekamalalamikoyakekwenyechombokinachoshughulikiakutatuamigogoroyauwekezaji cha kimataifa (ICSID). • Mwekezajiyeyoteanawezakukopakutokakwenyebenkiyeyotenchini. • Uwepowauwakilishimzuriwasektabinafsikama vile (TPSF) na (TNBC)
Fursa za Uwekezaji Nchini Zipo Fursa kadha wa kadha za uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali kama vile: • Kilimo na ufugaji • Uchimbaji na usafishaji Madini • Utengenezaji wa Miundombinu-barabara, bandari, na viwanja vya ndege • Utengenezaji Bidhaa za Viwandani • Ujenzi wa majumba ya biashara kama vile mahoteli na makazi • Huduma za utalii • Usafirishaji, n.k • Kujenga mashule,hospital • Kuweka miundombinu ya maji
Mwenendo wa Miradi Iliyoandikishwa na Tic Kuanzia 2005 to 2012 Mwaka Source: TIC data
UmilikiwaMiradiIliyoandikishwanaTIC 2005 - 2012 Source; Tanzania Investment Centre, 2012
Mwenendo wa Mitaji Kutoka Nje Kuanzia 2007 – 2012 (Us$ Mill) Source: UNCTAD - World Investment Report – 2013
Mikakati ya Kuvutia Uwekezaji • Kwa kushirkianan na taasisi za serikali na wadau wengine TIC inaendelea kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi. • Taasisi imeboresha tovuti yake (www.tic.co.tz) na kuizindua upya mwanzoni mwa mwaka huu ili kuimarisha upatikanaji wa taarifa kuhusu uwekezazi nchini • TIC huratibu na kuendesha makongamano ya mara kwa mara ya uwekezaji (Katavi-2012, Tanga-2013, Mwanza- 2014) • Kituo kimeingia mikataba ya ushirikiano na serikali za Mikoa ili kuboresha huduma kwa wawekezaji hususani upatikanaji wa ardhi
Mikakati ya Kuvutia Uwekezaji • TIC inatoa kipaumbele katika kutoa vivutio vya uwekezaji hasa kwa miradi ile yenye kuongeza dhamani bidhaa na huduma na kutoa ajira nyingi zaidi • TIC inashirikiana kwa ukaribu sana na Wizara ya Ardhi na serikali za Wilaya na Mikoa katika kuwatafutia Ardhi wawekezaji (Mfano: Kampuni ya NITOR(Japan)- Simiyu;) na vile vile Serikali imetenga Shamba la Mkulazi- Morogoro kwa ajili ya wawekezaji wa mpunga na miwa. • TIC ipo katika hatua ya mwisho ya mchakato wa kutoa huduma kwa wawekezaji kwa njia ya kielekroniki (E- Regulation) ikiwemo usajili wa kampuni, na TIN.
Mikakati ya Kuvutia Uwekezaji • TIC hutembelea miradi iliyosajiliwa ili kubaini maendeleo yaliyofikiwa na kutatua matatizo yanayoikabili kama yapo • TIC kwa kushirikia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) kuanzia mwaka 2009 inaandaa na kuendesha mafunzo maalumu ya ujasiriamali (Enterpreneurship Training Workshop (ETW) kwa wajasiriamali (SMEs) kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zao kisasa kama vile kuongeza ubora wa bidhaa. Jumla ya kampuni (SME) 350 kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Tanga, Mwanza, Mbeya zimenufaika na mafunzo haya
Changamoto • Ukosefu wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji • Migogoro ya ardhi • Miundombinu mibovu • Kutokurasimisha biashara baadhi ya wafanyabiasha • Utekelezaji wa mafunzo • Ukosefu wa utafiti • Uelewa hasi juu ya uwekezaji miongoni mwa wananchi
Mwisho • Pamoja na kuwepo kwa mikakati mbalimbali ya kuvutia uwekezaji. Kunahitajika kuwe na juhudi za pamoja za kuondoa vikwazo vyote vya kuwekeza katika sekta zote hapa nchini. Asanteni kwa kunisikiliza
Kwamawasilianozaiditumiaanuanihii:- Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwekezaji (TIC) P.O.Box 938 Dar es Salaam Tel: +255 22 2116328-32 Fax: +255 22 2118253 Email: information@tic.co.tz Website: www.tic.co.tz